*Mdee, Kubenea wakamatwa, Simbachawene atoa neno>>>>Mahakama yakana kuzuia uchaguzi wa Meya Dar Soma Zaidi Hapa>>>>>
Hakimu: Zuio umeya Dar feki *Mdee, Kubenea wakamatwa, Simbachawene neno NA WAANDISHI WETU, DAR ES SALAAM MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema hakuna amri iliyotolewa kuzuia Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliotakiwa kufanyika Februari 26, mwaka huu. Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Waliarwande Lema, alisema hayo jana alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu amri hiyo aliyodaiwa kuito kuzuia uchaguzi huo. “Hakuna amri ya kuzuia uchaguzi wa meya, aliyesema mahakama imetoa zuio ni muongo,” alisema Hakimu Lema. HAKIMU MFAWIDHI KISUTU Awali mapema asubuhi jana, waandishi wa habari za mahakama waliwasili ofisini kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Cysprian Mkeha kutaka ufafanuzi kuhusu zuio linalodaiwa kutolewa na mahakama hiyo kuzuia uchaguzi huo wa meya. Hakimu Mkeha, alisema Februari 25, mwaka huu hadi anaondoka kazini hakukuwa na maombi yoyote yaliyowasilishwa kupinga Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam. Alisema ...