Posts

Showing posts with the label SIASA

KAULI za Angelina Mabula baada ya kuteuliwa nafasi ya unaibu waziri na Rais MAGUFULI…

Image
Dec 10 Rais wa awamo ya tano Dr.John Pombe Magufuli aliteuwa rasmi baraza la mawaziri, miongoni waliotajwa ni mbunge wa Ilemela Angelina Mabula ambaye aliteuliwa katika nafasi ya naibu waziri wa Ardhi. Sasa mbunge huyo amefanya exclusive interview na ripota wa millardayo.com baada ya kuteuliwa katika nafasi hiyo ya kuwa naibu waziri…’ Kwanza namshukuru Mungu…pili namshukuru Rais wa awamo ya tano kunichagua katika nafasi ya unaibu kwa wana ilemela niseme tu kwamba nawashukuru tu wao kwasababu wasingenipa nafasi ya ubunge nisingefika hapa nilipo kwahiyo ningependa kuwaambia kwamba tupo bega kwa bega’ – Angelina ‘Naomba nikuhakikishia kwamba mimi sio kati ya wale wanaojisahahu kwasababu  dhamana hii niliyopewa ya unaibu waziri ina mikono ya wana ilemela kwahiyo niseme kwamba nitakuwa pamoja maana unapokuwa waziri au naibu waziri kuna vipindi ambavyo vipo unatakiwa kuwa jimboni…sikutarajia nafasi ya kuwa naibu waziri ila k...

chadema » Edward Lowassa » CHADEMA kumleta Lowassa ni Sawa Kujichimbia Kaburi la Kisiasa

Image
CHADEMA kumleta Lowassa ni Sawa Kujichimbia Kaburi la Kisiasa   Hayawi hayawi sasa yamekuwa, ule utabiri wetu kwamba iwapo Wana CHADEMA wataendelea kutii matakwa ya viongozi wao kwa staili ya ndio mzee itawazamisha wao na CHADEMA kwa ujumla sasa unaelekea kutumia. Laiti wana CHADEMA wangejenga utamaduni wa kuhoji kila uamuzi unaofanywa na viongozi wao, wakapinga au kukubali maamuzi hayo baada ya mijadala ya kina haya yasingetokea. Kitendo cha CHADEMA kumkaribisha Waziri mkuu mstaafu mh Edward Lowassa kumechafua hali ya hewa ya kisiasa ndani ya chama. Nakumbuka maneno aliyowahi kuyatamka Katibu Mkuu wa zamani wa CHADEMA Dr Slaa kwamba kitendo cha CHADEMA kumleta Edward Lowassa ndani ya chama ni sawa na kuchota kinyesi na kukihamishia chumbani, hii haimaanishi kwamba Lowassa mwenyewe ni mchafu (fisadi) ila msururu wa marafiki zake wenye kashfa lukuki za ufisadi ndio wangekichafua chama. Habari za kuibuliwa kwa tuhuma za watu walioshiri...

CHADEMA Wasema Magufuli Anatekeleza Sera za Wapinzani

Image
Wakati Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, John Magufuli akionekana kuteka hisia za Watanzania wengi, Chama  cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  kimesema hakishtushwi kwani amekuwa akitumia  hoja, mikakati na Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho. Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu, amesema kuwa wakati wa kampeni Chadema ilieleza jinsi ya kupambana na  ufisadi, kuwa na utaratibu bora wa utendaji kazi, uadilifu na uzembe wa watumishi wa umma, mambo ambayo sasa yanafanywa na Dk Magufuli. Hata hivyo, alisema kwa kuwa anachofanya hakikuwamo katika mipango ya Chama cha Mapinduzi (CCM), anaamini atakumbana na changamoto siku zijazo.  “Akiomba ushauri tutatoa kwa maana namna gani atekeleze, lakini ni mapema mno kusema kama ana dhamira ya kuyafanya. Pengine anayafanya kwa ajili ya kujitafutia umaarufu wa harakaharaka,” alisema Mwalimu. Mikakati ya Dk Magufuli Tangu Novemba 5 mpaka sasa, Dk Magufuli ametangaza mikakati kadhaa ya kubana matumizi ya ...

Dr Slaa » Dk. Slaa Atoka Mafichoni 'Nadhani Sasa Mnanielewa Niliposhikilia Msimamo Wangu'

Image
Dk. Slaa Atoka Mafichoni 'Nadhani Sasa Mnanielewa Niliposhikilia Msimamo Wangu' Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa amesifia kasi ya rais John Magufuli hasa katika kupambana na ufisadi nchini. Dk. Slaa amesema kuwa alichowahi kukizungumzia awali kimetimia kwa kuwa nchi hii ilihitaji mtu kama Magufuli. “ Nadhani sasa unaelewa niliposhikilia msimamo wangu. Katika mazingira ya sasa Magufuli ni bora zaidi. Niliwahi kusema kuwa hii nchi kwa siku za mwanzo inahitaji udikteta kuirudisha kwenye mstari ulioonyooka, nimefurahi sana ,” Dk. Slaa ameliabia gazeti la Raia Mwema. Amesema kuwa Bunge linatakiwa kufanya kazi ya kuudhibiti udikteta huo ili usivuke mipaka lakini limuunge mkono kwa hatua anazochukua. Katika hatua nyingine, Dk. Slaa amemshauri Rais Magufuli kuiangalia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kuifumua. “ Pasipo kuchukua hatua ya kuifumua Takukuru, sina hakika kama matarajio yatafikiwa ,” alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa hatua hizo z...

Kafulila Aanza Vizuri Kesi Yake Ya Kupinga Matokeo Ya Ubunge Baada Ya Pingamizi Kutupiliwa Mbali Na Mahakama

Image
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora inayosikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Kigoma Kusini iliyofunguliwa na David Kafulila dhidi ya washtakiwa; Husna Mwilima, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya uvinza kama msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria mkuu wa Serikali ilipokea pingamizi toka kwa wakili wa Husna Mwilima kutaka Mahakama Kuu isiendelee na kesi hiyo kwakuwa Mhe Kafulila hakufuata taratibu katika ufunguzi wa kesi hiyo. Katika utetezi wa mawakili wa Kafulila ambao  ni Daniel Lumenyera na Tundu Lissu waliomba mahakama itupilie mbali pingamizi hilo la wakili maarufu Fungamtama kwa hoja kuwa ni usumbufu kwa mteja wao na halina mana yoyote kwa kesi ya Msingi. Jana Jaji anayesikiliza kesi hiyo Bi Leila  Mgonya a li zingatia ombi la Fungamtama na utetezi Lumenyela na kuamua kutupilia mbali pingamizi hilo la wakili wa Husna na kumtaka Husna Mwilima kumlipa Kafulila gharama za usumbufu kwa kuweka mapingamizi yenye sura ya kupoteza muda na usumbufu. Ai...

Nape Nnauye » Nape Nnauye Awakata Watu Mdomo Wanaosema CCM Haiungi Mkono Juhudi Anazofanya Rais Magufuli...Asema Haya

Image
Nape Nnauye Awakata Watu Mdomo Wanaosema CCM Haiungi Mkono Juhudi Anazofanya Rais Magufuli...Asema Haya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema, kitampa ushirikiano mkubwa, Rais Dk. John Magufuli, ili aweze kwa ufanisi zaidi mapambano yake dhidi ya mafisadi na mikakati mingine ya kuinua uchumi wa Watanzania. Kimesema, kitampa ushirikiano huo Rais Dk. Magufuli, kwa sababu, aliyoanza kuyafanya na atakayoyafanya baadaye katika uongozi wake wa Urais anatekeleza yale yaliyomo katika ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020. Hayo yalisemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipokuwa akijibu maswali kadhaa yaliyoulizwa na baadhi ya wahariri, aliokuwa akizungumza nao, katika ziara aliyofanya leo, katika Kampuni ya New Habari Corporation, Sinza jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wahariri, waliohoji ni kwa nini CCM haijitokezi kumpongeza Dk. Magufuli katika juhudi ambazo ameanza kuonyesha katika kupambana na ufisadi ikiwemo kubana fedha za walipa kodi ambazo zingepotea bure katik...