Posts

Showing posts with the label KIMATAIFA

Burundi yafanyiwa kikao Addis

Image
  Burundi yafanyiwa kikao Addis Ababa  Mabalozi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanafanya mazungumzo kuhusu msukosuko wa Burundi na viongozi wa Umoja wa Afrika katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. Mkutano huo unafanywa siku moja baada ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa kukutana na rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, ambaye uamuzi wake wa kugombea muhula wa tatu wa uongozi ulizusha miezi kadha ya ghasia. Mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Samantha Power, alisema mazungumzo hayo hayakufanikiwa kama alivyotaraji. Rais Nkurunziza alikataa wito wa mazungumzo, upatanishi na kikosi cha Umoja wa Afrika kuingilia kati.

Mugabe "mzima kama kigongo"

Image
  Rais Robert Mugabe asema ni mzima kama kigongo    Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amerudi nyumbani baada ya likizo ya mwezi mmoja nchi za nje, juma moja baada ya wakuu kukanusha ripoti kwamba alishikwa na ugonjwa wa moyo. Bwana Mugabe, mwenye umri wa miaka 91, alisema ni mzima kama kigongo. Anakutana na kiongozi mwengine mkongwe wa Afrika, Teodoro Obiang Nguema wa Equatorial Guinea, ambaye anafanya ziara rasmi nchini Zimbabwe. Rais Nguema ameongoza Equatorial Guinea kwa miaka 36, mwaka mmoja zaidi ya Rais Mugabe.

Waziri Mkuu wa muda wa Uhispania amekataa ombo la kuunda Serikali mpya.

Image
    Waziri mkuu wa Uhispania Mariana Rajoy    Waziri Mkuu wa muda wa Uhispania amekataa ombo la kuunda Serikali mpya. Bwana Rajoy, ambaye chama chake kisichopendelea mabadiliko cha Popular Party kilishinda viti vingi vya Bunge, bila kuwa na idadi ya kutosha ya kuunda Serikali, katika uchaguzi wa mwezi uliopita, alikataa ombi la Mfalme Filipe kuwa aunde Serikali. Kwa mara ya kwanza tangu demokrasia irejee nchini Uhispania, Mfalme alikuwa mwenyekiti wa mkutano ulioshirikisha vyama vya kisiasa vinavyopingana Pedro Sanchez                                                                                                                ...

Kimbunga kikali chawasili Marekani mashariki

Image
Ajali zilizosababishwa na kimbunga hicho                                                                                            Kimbunga kikali cha theluji kinachobashiriwa kuwa kikubwa zaidi kwa muda wa miaka mia moja kimewasili katika ufukwe wa Mashariki mwa Marekani. Eneo linalotarajiwa kukabiliwa vikali ni mji mkuu wa Washington DC, ambako hali ya hatari tayari imetangazwa. Afisi za wafanya kazi wa Serikali na shule zilifungwa mapema na huduma za usafirishaji pia kusitishwa. Kimbunga nchini Marekani                                   ...

Mauwaji Mpya yatokea Canada Wanne wauawa katika ufyatulianaji risasi

Image
Eneo la tukio la ufyatulianaji wa risasi nchini Canada    Polisi nchini Canada wamesema kuwa watu wanne wameuawa katika ufyatulianaji wa risasi katika shule moja katika Mkoa wa Saskachewan, katikati mwa Canada. Ripoto za awali zilikuwa zimesema ni watu watano waliofariki. Mshukiwa mwanamume ametiwa mbaroni nje ya Shule ya Kijamii ya Loche, ambako kisa hicho kilitokea. Polisi pia wanaendelea kufanya uchunguzi katika tulio jingine la ufyatulianaji risasi katika kijiji cha watu 3,000 nchini humo. Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudea, ametaja vifo hivyo kama hofu kubwa inayoweza kumkumba mzazi yeyote. Mauaji ya watu wengi kwa bunduki nchini Canada si jambo la kawaida , ambako sheria za kuthibiti bunduki ni kali zaidi kuliko Marekani.

Maafisa wa Afya wa Brazil wanasema kuwa wanahofia kwamba maradhi yanayoenezwa na mbu ya virusi vya Zika huenda yameenea kuliko walivyotarajia.

Image
  Watoto walioathirika na Zika    Maafisa wa Afya wa Brazil wanasema kuwa wanahofia kwamba maradhi yanayoenezwa na mbu ya virusi vya Zika huenda yameenea kuliko walivyotarajia. Virusi hivyo vimedaiwa kusababisha ongezeko la ulemavu miongoni mwa watoto wadogo wanaozaliwa nchini humo. Hofu imetanda wakati huu ambapo mji mkuu wa Rio unatarajia kuwa mwenyeji wa michezo ya Olympiki mwaka huu. Kukabiliana na virusi vya Zika    Watafiti wamesema kuwa hali ya hewa yenye unyevu mkubwa ndiyo iliyochangia pakubwa mlipuko wa maradhi hayo. Kampeni ya kuwahamasisha wananchi kuyaondoa maji yaliyosimama, ambako mbu wanazaana imeanzishwa huku juhudi za kubuni chanjo zikiendelea. Idara ya Afya nchini Marekani imewaonya wanawake waja wazito wasitembelee mataifa 20 katika eneo la Brazil, kukiwemo sehemu zingine kama vile visiwa vya Samoa na Cape Verde. Mbu wanaosababisha ugonjwa h...

Misri yatofautiana na IS kuhusu shambulio

Image
  Rais Abdel Fattah al Sisi    Kundi la Islamic State limekiri kutekeleza shambulio katika mji wa Cairo nchini Misri ambalo liliwaua takriban watu tisa wengi wao wakiwa maafisa wa polisi. Lakini mamlaka imesema kuwa mlipuko huo ulitokea wakati wa uvamizi siku ya Alhamisi katika maficho yanayotumiwa na wapiganaji wa kundi la Muslim Shambulio Misri     Zaidi ya watu 13 walijeruhiwa akiwemo afisa mkuu wa polisi katika eneo la Giza,ambalo liko karibu na eneo maarufu lenye piramidi. Serikali imeimarisha usalama huku taifa hilo likikaribia kuadhimisha miaka mitano ya mapinduzi yaliomuondoa rais wa muda mrefu wa taifa hilo Hosni Mubarak. Wapiganaji wa Islamic State    Vuguvugu la Muslim brotherhood,ambalo ndilo lililomuweka aliyekuwa rais Mohammed Morsi ambaye alichagliwa baada ya mapinduzi ilipigwa marufuku.

Sudan yaipunguzia ada Sudan Kusini

Image
Sudan Kusini hulazimika kutumia mabomba ya mafuta ya Sudan kuweza kuuza mafuta yake nje  Sudan imekubali kupunguza ada inayotosa jirani wake Sudan Kusini kusafirisha mafuta kupitia kwa mabomba yake.  Nchi zote mbili zimekuwa zikitofautiana kuhusu ada hiyo ambayo imetishia kuangamiza sekta ya mafuta ya Sudan Kusini baada ya mzozo wa hivi majuzi.   Wakati Sudan Kusni ilipopata uhuru wake pia ilipata maeneo yenye utajiri wa mafuta lakini huwa inalazimika kutumia mabomba ya mafuta ya Sudan kuweza kuuza mafuta yake nje.  Ada inayotoswa na Sudan kusafirisha mafuta ya Sudan Kusini ni dola 24 kwa pipa, na wakati bei ya sasa ya mafuta ni dola 30 kwa pipa, suala hilo limeiathiri pakubwa Sudan Kusini.

Mwanafunzi Mmarekani akamatwa Korea Kaskazini

Image
Uhusiano kati ya Korea Kaskazini na nchi za Magharibi umeendelea kudorora                                  Korea Kaskazini imesema imemkamata mwanafunzi kutoka Marekani ambaye anadaiwa kufanya “kitendo cha uchokozi” dhidi ya taifa. Shirika la habari la serikali KCNA limesema serikali ya Marekani ilikuwa “imemvumilia na kumtawala kwa werevy” mwanafunzi huyo, ambaye husomea Chuo Kikuu cha Virginia. Mwanafunzi huyo ambaye jina lake halijatolewa anadaiwa kuingia Korea Kaskazini kama mtalii, na inadaiwa “alilenga kuvunja umoja wa taifa hilo”. KCNA haijatoa maelezo zaidi, lakini mwanafunzi huyo anaendelea kuchunguzwa. Mhubiri wa Canada afungwa maisha Korea Kaskazini UN kuichukulia hatua Korea Kaskazini Afisa wa ubalozi wa Marekani katika taifa jirani la Korea Kusini ameambia shirika la habari la Reuters kwamba hawana habari kuhusu kuka...

Kenyatta azuru waliojeruhiwa uvamizi wa al-Shabab

Image
Rais Kenyatta ameahidi kuwaandama walioshambulia kambi ya el-Adde                                                                  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anawatembelea wanajeshi waliojeruhiwa baada ya wanamgambo wa al-Shabab kushambulia kambi ya wanajeshi nchini Somalia Ijumaa iliyopita. Rais Kenyatta atatembelea majeruhi hospitali ya Forces Memorial, Nairobi na baadaye kujumuika na jamaa, marafiki na maafisa wakuu wa jeshi kwa ibada ya kuwakumbuka wanajeshi waliouawa. Wanajeshi tayari wamekusanyika ndani ya hospitali hiyo ya majeshi                                                               ...

HAYA NDIO MANENO YA SIRI YALIO TUMIWA ZAIDI 2015 >>>Nywila (Maneno Ya Siri) zilizotumiwa sana na watu 2015

Image
Filamu ya Star Wars ilivuma sana baada ya kuzinduliwa Desemba                                                                               Kampuni ya usalama mtandaoni ya SplashData imetoa orodha ya nywila au maneno ya siri yaliyotumiwa sana na watu mwaka uliopita. Orodha hiyo imetayarishwa kwa kutumia maneno ya siri zaidi ya milioni mbili yaliyofichuliwa na wadukuzi mwaka uliopita. Mwaka huu, neno ‘Star Wars’, kutoka kwa mwendelezo wa filamu za Star Wars, lilikuwa miongoni mwa maneno 25 yaliyotumiwa zaidi. Filamu ya Star Wars: The Force Awakens ilizinduliwa mwezi Desemba. Wengi bado wanatumia ‘123456’ kama nywila na wengine ‘password’. Ili kuwa salama mtandaoni, huwa ni vyema kutumia nyila ambayo watu wengine hawawezi wakaifikiria au kugundua k...

Bomu lalipuka katika mgahawa Somalia

Image
somalia                                                                                                                                                 Bomu lililotegwa ndani ya gari limelipuka nje ya mgahawa mmoja uliopo katika ufukwe wa bahari katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu,kulingana na maafisa wa polisi. Walioshuhudia wamemwelezea mwandishi wa BBC Ibrahim Aden kwamba gari hilo lililojaa vilipuzi liligonga mgahawa huo maarufu wa Lido Beach kabla ya watu watano kujitokeza na kuanza kufyatua risasi. Haijulikani iwapo kumekuwa na majeruhi. Hakuna kundi lililokiri kutekeleza shambu...

Mauaji ya kale yagunduliwa Turkana Kenya : Soma zaidi hapa

Image
Mabaki ya watuo waliofariki yapata miaka 6000 iliopita katika ziwa Turkana nchini Kenya             Wanakiolojia wamepata ushahidi kaskazini mwa Kenya katika kile huenda ni mfano wa vita kati ya jamii tofauti. Mabaki hayo ya miaka 10,000 kutoka kwa watu 27 ambayo yalipatikana magharibi mwa Ziwa Turkana yanaonyesha kuwa yalisababishwa na mauaji. Waliwachwa kufa katika eneo hilo badala ya kuzikwa.Wataalamu wengi walidhani mgogoro huo ulitokea yapata miaka 6000 baada ya raia kupata makaazi. Wanakiolojia hao ambao wamekuwa wakifanya kazi katika eneo hilo la Nataruk tangu mwaka 2012,waligundua kwamba waathiriwa walichapwa ama hata kudungwa visu kwa pamoja. Waliouawa ni wanaume na wanawake pamoja na watoto. Ushahidi,uliochapshwa katika jarida la asili hauonyeshi kile kilichotokea lakini ni kitu kilichosababishwa na mgogoro kulingana na profesa Robert Foley wa Chuo kikuu cha Cambridge.

Huenda rais Putin 'aliidhinisha' mauaji ya Jasusi :SOMA ZAIDI HAPA

Image
Litvinenko                                                                                                                                              Mauaji ya aliyekuwa jasusi wa Urusi Alexander Litvinenko mwaka 2006 nchini Uingereza huenda yaliidhinishwa na rais Vladimir Putin ,kulingana na uchunguzi. Bwana Putin huenda alitia saini sumu ya mauaji ya bwana Litvinenko ya polonium-210 kutokana na uhasama kati yao, ulisema uchunguzi. Mjane wa Bwana Litvinenko,Marina aliunga mkono ripoti hiyo akitaka bwana Putin kuwekewa marufuku ya usafiri huku Urusi ikiwekewa vikwazo. Hatahivyo waziri wa maswala ya kigeni wa Urusi ame...

Maajabu..Mwanamke Akutwa Chini ya Shimo la Choo...Inasemekana Aliwekwa Kama Msukule..Samahani kwa Picha

Image
Picha hizi Zinasambaa Mtandaoni hasa Instagram zikimuonyesha Mwanamke akiwa hivyo Inasemekana Mwanamke huyo amekutwa ndani ya chemba (sewage) ya Mkazi/Mfanyabiashara Mchagga wa Kibamba aliyejulikana kwa jina la Mtei. Amefikaje? Haikufahamika ila walisikika wananchi wakisema ni msukule.dunia ina mambo hii duuuuu Tunafatilia Habari Kamili kisa cha huyo dada kuishi ndani ya Shimo la choo..                                               KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI

Lupita Nyong'o » Oscar » George Clooney, Lupita Nyong’o Waungana na Spike Lee na Jada Pinkett Kulalamikia Tuzo za Oscar Kutawaliwa na Watu Weupe

Image
Washindi wa tuzo za Oscar, George Clooney na Mkenya, Lupita Nyong’o pamoja na muigizaji wa Uingereza David Oyelowo wameungana na mastaa wengine waliopaza sauti kutaka kuwepo mabadiliko kwenye tasnia ya filamu na akademi ya sanaa ya picha zitembeazo na sayansi ambayo wajumbe wake walitaja majina ya waigizaji weupe tu kwenye tuzo za Oscars 2016 kwa mwaka wa pili mfululizo. Clooney alisema kuwa Academy ilikuwa ikifanya vizuri zaidi miaka 10 iliyopita ambapo waigizaji weusi walikuwa wakipata nafasi. Muongozaji wa filamu Spike Lee, anayeongoza wito wa kuzisusia tuzo hizo ametaka kuwepo kwa hatua stahiki ili kuleta usawa katika matabaka mbalimbali kwenye Hollywood. Lee, aliyewahi kupewa tuzo ya heshima ya Oscar, amedai kuwa Hollywood ipo nyuma ya muziki na michezo katika kutambua watu wa matabaka mengine tofauti na weupe. Mwingine aliyepo mstari wa mbele ni Jada Pinkett-Smith, mke wa Will Smith aliyeigiza filamu ya Concussion ambayo haijatajwa kwenye tuzo hizo...

WHATSAPP KUTUMIWA BURE >>>> SOMA ZAIDI HAPA>>>

Image
Wanaotumia WhatsApp hutakiwa kulipa dola moja baada ya mwaka mmoja                                       Wamiliki wa app ya mawasiliano ya WhatsApp wamefuta ada ambayo watumizi wake wamekuwa wakitakiwa kulipa kila baada ya mwaka mmoja. Wamiliki wa huduma hiyo wamekuwa wakiwatoza watu $0.99 kila mwaka baada ya kuitumia kwa mwaka mmoja. Ada hiyo ilianza kutozwa miaka michache iliyopita lakini kampuni hiyo inasema haijakuwa na manufaa sana. Taarifa kutoka kwa wamiliki wa WhatsApp inasema: “Watu wengi wanaotumia WhatsApp hawana kadi za benki na wengine huwa na wasiwasi kwamba baada ya mwaka mmoja watazuiwa kuungana tena na marafiki na jamaa.” “Kwa hivyo, wiki chache zijazo, tutaondoa ada zote tunazotoza wa wanaotumia aina mbalimbali za app yetu na hutatozwa tena pesa ili kutumia WhatsApp.” Kwa sasa, WhatsApp, ambayo humilikiwa na Facebook, hutumiwa na watu bilioni moja na k...

Japan YAMPOTE MZEE MWENYE UMRI MKUBWA ZAIDI DUNIANI akiwa na umri wa miaka 112 SOMA ZAIDI HAPA>>>

Image
 JAPANA YAMPOTE MZEE MWENYE UMRI MKUBWA ZAIDI DUNIANI ALIKUWA NA MIAKA 112 SOMA ZAIDI HAPA>>>  MAREHEMU Yasutaro Koide                                                                    Mwanamume mkongwe zaidi duniani amefariki nchini Japan akiwa na umri wa miaka 112. Yasutaro Koide, kutoka jiji la Nagoya, alizaliwa tarehe 13 Machi 1903 na alifanya kazi kama fundi wa nguo wakati wa ujana wake. Alitambuliwa na Guiness Book of World Records kama mwanamume mzee zaidi duniani Agosti mwaka jana. Yasutaro alifariki kutokana na maradhi ya moyo na nimonia mapema Jumanne. Alipoulizwa kuhusu siri ya maisha marefu alipokuwa hai, anadaiw...

Iran imepuuzilia mbali vikwazo vipya dhidi yake ilivyowekewa na Marekani kuhusu mpango wake wa kutengeza makombora.

Image
Vikwazo hivyo havina 'uhalali wa kisheria wala wa kimaadili',msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni amesema. Mnamo mwezi Oktoba ,Iran ililifanyia jaribio kombora lake lililo na uwezo wa kubeba kichwa cha kombora la nuklia,ikikiuka marufuku ya Umoja wa mataifa. Hatua hiyo ya Marekani inajiri baada ya vikwazo ilivyowekewa Iran kuondolewa kufuatia mkataba wa mpango wake wa nuklia. Vikwazo hivyo vipya vitawazuia watu na makampuni 11 wanaohusishwa na mpango huo wa kutengeza makombora kutotumia mfumo wa benki wa Marekani.

Mkumbuke Mungu Kwa kila jambo"🙏

Image
MKIMPENDA MUNGU MTAZISHIKA AMRI ZAKE NAZO SIO NZITO NA MWINJILIST NIKODEM PAUL KIRUMBA SDA MWANZA KATIBA ISIYOHITAJI MAREKEBISHO Tunashuhudia katika nchi nyingi kilio cha kutaka katiba zilizopo zirekebishwe. Madai hayo yalikuwepo hata hapa Tanzania jambo lililomfanya rais wa nchi kuunda tume ya kukusanya maoni ya wananchi kwa lengo la kuirekebisha katiba iliyopo. Mchakato huo unaendelea na tunauombea ufikie hatua ya kukidhi matarajio ya walio wengi. Lakini mtu aweza kujiuliza katiba ni nini? Kwa maelezo rahisi katiba ni makubaliano baina ya watawala na watawaliwa. Mungu naye anayo katiba inayoelekeza mahusiano baina yake yeye aliye mtawala na wanadamu walio watawaliwa. Makubaliano hayo yanapatikana kwenye kitabu maarufu kilichobadili maisha ya watu kwa maelfu kiitwacho Biblia. Makubaliano haya yanaainisha wajibu na haki za kila upande. Kwa upande wa Mungu anamwagiza mwanadamu kutii maagizo yake kwa faida yake yeye mwenyewe mwandamu na mustakabali mwema wa maisha yake. Kwa upande wa mwa...