Kenyatta azuru waliojeruhiwa uvamizi wa al-Shabab

KenyattaRais Kenyatta ameahidi kuwaandama walioshambulia kambi ya el-Adde                                                                 


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anawatembelea wanajeshi waliojeruhiwa baada ya wanamgambo wa al-Shabab kushambulia kambi ya wanajeshi nchini Somalia Ijumaa iliyopita.

Rais Kenyatta atatembelea majeruhi hospitali ya Forces Memorial, Nairobi na baadaye kujumuika na jamaa, marafiki na maafisa wakuu wa jeshi kwa ibada ya kuwakumbuka wanajeshi waliouawa.

MajeshiWanajeshi tayari wamekusanyika ndani ya hospitali hiyo ya majeshi                                                                                       

Serikali ya Kenya bado haijatoa idadi kamili ya wanajeshi wake walioua wa baada ya kambi hiyo iliyoko el-Ade kushambuliwa.

Kundi la al-Shabab awali lilisema liliwaua wanajeshi zaidi ya 60 wa Kenya.
Mamia ya jamaa na marafiki wamekuwa wakifika katika vituo vilivyotengwa na idara ya jeshi nchini Kenya kutafuta habari kuhusu wapendwa wao.

Mkuu wa jeshi Jenerali Samson Mwathethe aliambia wanahabari Alhamisi kwamba jeshi bado linaendelea kukusanya habari kuhusu wanajeshi waliokuwa kwenye kambi hiyo.

MajeshiBaadhi ya wanajeshi waliojeruhiwa wanatibiwa katika hospitali ya majeshi                                        

Alidokeza pia kwamba huenda ikabidi uchunguzi wa vijinasaba kufanywa kutambua miili ya baadhi ya wanajeshi waliouawa.

Alisema bomu lililotumiwa na washambuliaji hao kuvamia kambi hiyo lilikuwa na nguvu mara tatu kushinda bomu lililotumiwa kushambulia ubalozi wa Marekani jijini Nairobi mwaka 1998.

Watu takriban 250 waliuawa kwenye shambulio hilo.


Comments

Popular posts from this blog

TAZAMA PICHA 30 ZA MREMBO AGNES MASOGANGE AKIJIACHIA KISTAA NJE YA NCHI

Gamboshi: Makao Makuu ya Uchawi na Wachawi yaliyopo Shinyanga, Tanzania

14 parties want Parliament to discuss Zanzibar impasse