Posts

Showing posts with the label MICHEZO

Van Gaal aomba radhi kwa kujiangusha

Image
Van Gaal aomba radhi kwa kujiangusha MANCHESTER, ENGLAND KOCHA wa Manchester United, Van Gaal, ameomba radhi kwa kitendo cha kujiangusha juzi mbele ya mwamuzi wa akiba, Mike Dean, katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal, kwenye Uwanja wa Old Trafford. Kocha huyo alijiangusha kwa makusudi huku akiwa na lengo la kumuonesha mwamuzi jinsi wachezaji wa Arsenal wanavyojiangusha kwa kumdanganya mwamuzi wa mchezo huo. Kocha huyo alimwambia mwamuzi kwamba mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez, amekuwa mjanja hivyo mara kwa mara anajiangusha kwa ajili ya kuomba ili waweze kutumia mipira ya adhabu. Hata hivyo, Van Gaal amekiri kwamba alifanya makosa kuonesha mfano huo mbele ya mashabiki ambao walionekana kushangilia. “Halikuwa jambo zuri kufanya mbele ya mwamuzi wa kati, mshika kibendera na mwamuzi wa akiba, ninakubali kwamba nilifanya makosa na natumia muda huu kuomba radhi kwa kitendo ambacho nilikifanya, japokuwa mashabiki walionekana kuf...

Wenger ashitushwa na kiwango cha Rashford

Image
MANCHESTER, ENGLAND KOCHA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger, amedai kwamba ameshitushwa na uwezo wa nyota wa Manchester United, Marcus Rashford, aliouonesha juzi katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 18, juzi alionesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo huo dhidi ya Arsenal, ambapo alipachika mabao mawili ndani ya dakika tano katika kipindi cha kwanza kwenye ushindi wa mabao 3-2. Kutokana na kiwango hicho, Wenger amedai kwamba hakutarajia kuona uwezo mkubwa ambao aliuonesha mchezaji huyo. “Kwa upande wetu, tulishindwa kuwa na mipango mizuri ya kutafuta mabao kutokana na nafasi ambazo tulizipata, lakini katika mchezo huo nilikuja kushangazwa na uwezo wa nyota mpya wa Man United, Rashford. “Nadhani haikuwa kwangu tu, ilikuwa kwa kila mmoja kushangazwa na uwezo wa mchezaji huyo ambaye alifanikiwa kufunga mabao mawili, alikuwa na akili ya kwenda na mchezo na kujua wapi sehemu sahihi ya kukaa. “Ninaamini atakuja kuwa na u...
Image
Mourinho akaribia kutua Old Trafford Wamiliki wa Manchester United ndiyo wenye uamuzi wa mwisho wa kumtimua Louis van Gaal baada ya Jose Mourinho kukubali kuwa kocha mpya wa miamba hiyo ya Old Trafford. Mazungumzo yamefanyika kati ya klabu na Mourinho, na Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Man United, Ed Woodward amefanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa mbadala wa Van Gaa anapatikana pindi utakapohitajika. Kilichobaki sasa ni kwa familia ya Glazer kuamua kufanya mabadiliko hayo, na malumbano yaliyopo ni kumtimua Van Gaal sasa au kumpa nafasi ya mchezo ujao wa Jumamosi dhidi ya Stoke. Bodi ya Old Trafford imekuwa katika majadiliano ya kumtimua Mholanzi huyo, ambaye alionekana kama chaguo la kwanza baada ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson, ambaye alishauri aitwe David Moyes. Lakini kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Norwich Jumamosi kilikuwa cha tatu mfululizo kwa miamba hiyo ya Old Trafford na wasiwasi ni kwamba timu imekosa ari tena. Kumaliza ligi katika nafasi ya nn...

Mourinho hakutuma ombi la kazi Man Utd

Image
Mourinho hakutuma ombi la kazi Man Utd                                                                              Ripoti inayodai kuwa aliyekuwa meneja wa Chelsea,Jose Mourinho aliiandika Manchester United barua yenye kurasa sita akielezea upungufu wa kocha wa Man United Louis van Gaal imetajwa kuwa "ajabu kabisa", anasema wakala wake, Jorge Mendes. Jarida la Independent la Jumapili pia limedai Mourinho aliwasilisha "uchambuzi wa kisayansi" wa kikosi kizima cha Old Trafford katika kile kinachoitwa " barua ya upendo" kwa klabu hiyo. United walizomewa na mashabiki wao wa nyumbani hapo jana Jumamosi baada ya kulazwa bao 1-0 dhidi ya Southampton. Jarida la Independent la Jumapili pia limedai Mourinho aliwasilisha "uchambu...

Staa wa FC Barcelona ahukumiwa kwenda Jela Mwaka 1 kwa ukwepaji Kodi

Image
Staa wa FC Barcelona ahukumiwa kwenda Jela Mwaka 1 kwa ukwepaji Kodi Klabu ya FC Barcelona imekuwa na historia ya kuhusishwa na ukwepaji kodi mbalimbali kupitia wachezaji wake maarufu, akiwemo Lionel Messi, Neymar na Javier Mascherano, na hatimaye jana mahakama moja nchini Hispania imetoa hukumu ya kwenda Jela kwa mmoja wa mastaa wao. Story ya Javier Mascherano na kesi ya ukwepaji kodi imefikia tamati. Kama ilivyotegemewa, Muargentina huyo sasa itabidi alipe kiasi kikubwa cha faini baada ya kukubali kosa ya kukwepa kodi mwanzoni mwa mwaka. Mascherano ameamriwa kulipa faini ya €816,000 (£588,000), ambayo ni fedha nyingi sana – ukizingatia mchezaji huyo analipwa £130,000 kabla ya kodi. Mchezaji huyo pia amehukumia kifungo cha mwaka mmoja jela, lakini kama ilivyo kesi za watu wengi maarufu – Mascherano hatokwenda jela baada ya mawakili wake kufikia makubaliano maalum na mahakama na aaendesha mashtaka.

Man Utd wakana kukutana na Guardiola

Image
Guardiola ataondoka Bayern baada ya kumalizika kwa msimu huu                                                      Manchester United wamekanusha habari kwamba walikutana na kuzungumza na meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola kuhusu uwezekano wake kuwa meneja wao. Tovuti ya France Football ilikuwa imesema mkutano huo ulifanyika mjini Paris lakini United wamesema habari hizo si za kweli. Meneja wa sasa wa United Louis van Gaal amekabiliwa na shinikizo baada ya klabu hiyo kutofanya vyema ligini Uingereza na Ulaya.. Guardiola asema atahamia Uingereza Guardiola, 45, anataondoka Bayern Munich majira yajayo ya joto na amesema amepokea maombi kutoka kwa klabu kadha za Uingereza. Manchester City wamo kwenye nafasi nzuri ya kumchukua, lakini Chelsea na United wamedaiwa kumtafuta pia. Bayern Munich walikuwa kwenye ...

Mshambuliaji Mauro Zarate ameihama klabu ya West Ham inayocheza Ligi Kuu ya Uingereza na kujiunga na klabu ya Fiorentina ya Italia.

Image
Image caption Zarate alifungia West Ham mabao 21 msimu huu                                                          Mshambuliaji Mauro Zarate ameihama klabu ya West Ham inayocheza Ligi Kuu ya Uingereza na kujiunga na klabu ya Fiorentina ya Italia. Mchezaji huyo wa umri wa miaka 28 alijiunga na West Ham kutoka Velez Sarsfield majira ya joto 2014. Alitatizika kupata nafasi timu ya kwanza na baadaye akapelekwa QPR kwa mkopo. Zarate, ambaye ni mzaliwa wa Argentina, alirejea msimu huu na kufana sana Upton Park. Amefungia klabu hiyo mabao 21 msimu huu. "West Ham ingependa kumshukuru sana Mauro kwa juhudi zake akiwa na jezi za klabu hii na inamtakia kila la kheri,” klabu ya West Ham imesema kupitia taarifa.

Difenda wa Barcelona na Argentina Javier Mascherano kortini kuzuia kutupwa jela

Image
Mascherano alikuwa amekiri makosa mawili ya kukwepa kufichua mapato yake                                Difenda wa Barcelona na Argentina Javier Mascherano amefika mahakamani kujaribu kuzuia asitupwe jela kwa kosa la ulaghai katika ulipaji ushuru. Anadaiwa kutumia ulaghai kukwepa kulipa ushuru wa jumla ya euro1.5m (£1.1m). Mascherano, 31, awali alikiri makosa mawili ya kukosa kutangaza mapato yake kamili ya 2011 na 2012. Jaji atatoa uamuazi wa iwapo Mascherano anaweza kulipa faini ya juu ili asifungwe jela, kwa mujibu wa ripoti Uhispania. Anadaiwa kujaribu kutumia hila kuficha mapato kutoka kwa uuzaji wa haki za kutumia picha zake akitumia kampuni anazomiliki ng’ambo. Stakabadhi za mahakama zinaonyesha mchezaji huyo alilipa jumla ya euro 1.75m, kiasi kamili alichodaiwa pamoja na riba. Baada ya kufika kortini Catalonia, nyota huyo wa zamani wa Liverpool ...

Arsenal kuikabili Chelsea Ligi kuu England

Image
Chelsea kuchuana na Arsenal                                                                                                                                                                                                                                                                                       ...

UNAMJUA KINARA WA MAGOLI YANGA?>> SOMA HAPA KUMJUA

Image
Mshambuliaji wa Yanga, Hamisi Tambwe                                                                                                               Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Mrundi Hamisi Joselyn Tambwe ameendelea kuwa kinara wa kupachika mabao katika klabu yake ya wanajangwani Yanga SC. Tambwe amefanikiwa kuirejesha timu hiyo kileleni mwa Ligi kufuatia ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Timu ya Majimaji katika mchezo uliopigwa jana uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, yeye akipachika mabao 3 katika ushindi huo. Kwa ushindi huo Yanga imerudi tena kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa kufikisha alama 39, sawa na Azam FC iliyopo nafasi ya pili kwa wastani m...

Breaking News: Huyu Ndio Mchezaji Bora wa Dunia Aliyetangazwa Usiku wa Leo>> SOMA ZAIDI HAPA>

Image
Kura walizopata katika kinyang'anyiro cha Tuzo ya Mchezaji Bora Dunia 2015 1.Lionel Messi 41.33 % 2.Cristiano Ronaldo 27.76 % 3.Neymar Jr 7.86 % Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Barcelona, na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, ametwaa tuzo ya mchezo bora wa dunia. Messi mwenye miaka 28 alishinda kwa 41.33% kwa kura zote zilizopigwa, huku Cristiano Ronaldo akishika nafasi ya pili kwa 27.76% na Neymer akipata 7.86%. Hii ni mara yake ya tano kutwaa tuzo hiyo. Kwa upande wa wanawake nyota wa Marekani Carli Lloyd, ameibuka kuwa mchezaji bora kwa upande wa wanawake. Goli bora la mwaka likifahamika kama Puskas limwendea Wendell Lira anayekipiga katika Atletico Goianiense ya Brazil. Kocha wa Barcelona Muhispania Luis Enrique amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwaka kwa kuiongoza barca kufanya vizuri barani Ulaya kwa kutwa mataji matano msimu uliopita. Jill Ellis kocha wa kikosi cha taifa cha Marekani amekuwa kocha bora wa wanawake baada ya kuongoza timu ya taifa ya Marekani kufa...

Ijue sababu sababu inayomfanya Guardiola aondoke FC Bayern na kuthibisha kwenda nchi hii (+Video)

Image
Bado headlines za anayetajwa kuwa kocha ghali kwa sasa duniani Pep Guardiola anakwenda kufundisha klabu gani zinazidi kuchukua nafasi, tayari Pep Guardiola ametaja nchi atakayokwenda kufundisha soka baada ya kukiri kuwa hatoendelea na kuifundisha klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani . Pep Guardiola amekiri kuamua kuondoka ndani ya klabu ya FC Bayern , baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka mitatu, sababu zinazomfanya Guardiola aondoke klabu ya FC Bayern ni kuwa yeye bado kijana na anahitaji changamoto mpya katika maisha yake ya ukocha. Lakini Guardiola  kathibitisha kuwa asingependa kuustafu ukocha bila kufundisha klabu za Uingereza , hivyo kwa kauli hiyo tayari Guardiola anakuwa katoa uhakika wa kwenda Uingereza ila klabu bado haipo wazi atakayojiunga nayo ” Nafikiri mimi bado kijana, ndio kwanza nina umri wa miaka 44, nahitaji changamoto mpya na nisingependa kustaafu bila kufundisha soka Uingereza” >>> Guardiola

Michezo Cheki video ya Ronaldo, Bale, Ramos na wachezaji wengine wa Real Madrid wakimpokea Zidane

Image
Ikiwa ni siku chache zimepita toka uongozi wa Real Madrid utangaze kumfuta kazi aliyekuwa kocha wa timu hiyo  Rafael Benitez na nafasi yake kuchukuliwa na mkongwe wa zamani wa timu hiyo Zinedine Zidane . Zimenifikia video za Zidane alivyowasili katika vyumba vya kubadilishia nguo vya Real Madrid na kukutana na wachezaji wake kwa siku ya kwanza kama kocha wa timu hiyo, lakini pamoja na video ya mazoezi yake ya kwanza kama kocha wa timu hiyo.

Pamekucha >>>>>Zidane Ala shafu>>> Meneja mpya Madrid

Image
Rafael Benitez Uongozi wa klabu ya Real Madrid umemtimua kocha wake Rafael Benitez ambaye ana Miezi 7 tu katika Mkataba wake wa Miaka Mitatu, na nafasi yake imechukuliwa na mchezaji mkongwe mfaransa Zinedine Zidane zizou ambaye awali alikuwa Kocha wa Kikosi B cha timu hiyo . Hii inatokana na matokeo mabaya kwa timu hiyo, ambapo ilitoka Sare 2-2 na Valencia katika Mechi ya La Liga, Sare ambayo imewaacha Vigogo hao Nafasi ya 3 wakiwa nyuma ya Atletico Madrid kwa pointi 4. Tangu atue Madrid Benitez amekuwa si kipenzi cha Mashabiki wa Klabu hiyo, baada ya kufungwa bao 4-0 kwenye mechi ya El Clasico Mwezi Novemba na Mahasimu wao Barcelona , Pia kutupwa nje ya michuano ya Copa del Rey. Real ilitoka Sare 2-2 na Kikosi cha Gary Neville, Mchezaji wa zamani wa Man United ambae sasa anaifundisha Valencia, iliyotoka 2-2 na Real Uwanjani Mestalla katika Mechi ya La Liga, Sare ambayo imewaacha Vigogo hao Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Vinara Atletico Madrid. T...

MAN UTD BOSS LOUI VAN GAAL TO QUIT OLD TRAFFORD?

Image
The Dutchman, under pressure after seven games without a victory, was asked at his post-match news conference whether he feared he would be sacked. Van Gaal, 64, said that was something he would discuss with executive vice-chairman Ed Woodward and not the media. “It is not always the club that has to fire or sack me,” he said. “Sometimes I do that by myself, but I am the one who wants to speak first with the board of Manchester United and my members of staff and my players, not with you.” United’s miserable run has seen them knocked out of the Champions League at the group stage and slip out of the top four in the Premier League. Van Gaal, who succeeded David Moyes in the summer of 2014, said the club had backed him “all the time” but added: “We have lost so there is a new situation. “I feel the support of my players and my board. The fans will be disappointed but that is logical after four defeats.” Van Gaal does not think it is important that Woodward has not publi...

GUESS WHICH POSSIBLE FUTURE MAN UTD MANAGER IS HOLIDAYING IN KENYA?>>>>Kuna Taarifa zinasema Pep Guardiola yuko Mombasa katika mapumziko mafupi.>>>

Image
Critics are saying today’s #MANVsCHE match might just be the last match for Van Gaal at the reign of Manchester United. If he indeed loses and the inevitable happens then one particular coach will most likely be considered. Pep Gurdiola, out going coach of Bayern Munich will be watching the game from the coastal shores of Mombasa. Karibu Pep!

Mtanange wa kukata na Soka>>>>> Nani Zaidiiiiiii

Image

Hii ndio Video yenyewe mtu wangu ya dakika 1 na sekunde 58

Image
Wachezaji soka wa Ulaya ni watu ambao wasiri sana katika maisha yao, kutokana na umaarufu wao mara nyingi wamekuwa wakifuatiliwa kwa kila kitu wanachokifanya, Cristiano Ronaldo staa wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid ya Hispania , December 22 kuekea sikuku ya Chrismass ameonesha mjengo wake kuanzia nje hadi ndani. Kama ulikuwa hujui Ronaldo sehemu muhimu katika nyumba yake ni mahali anapolala kwani ndio anaamini kama mchezaji ili ufanye vizuri ni lazima upate mahali pazuri pakupumzika. Najua umezoea kuona pichaz za mijengo ya mastaa wa soka, ila December 22 Ronaldo katuonesha mjengo wake na kutoa maelezo hadi chumbani anapolala. Hii ndio Video yenyewe mtu wangu ya dakika 1 na sekunde 58

FIFA: Blatter na Platini nje kwa miaka 8

Image
               Blatter na Platini nje kwa mika 8 Maafisa wawili wakuu zaidi katika usimamizi wa kandanda duniani rais Sepp Blatter na mwenyekiti wa shirikisho la soka barani ulaya UEFA Michel Platini, wamepigwa marufuku ya miaka 8 ya kutoshiriki kwa vyovyote maswala ya soka kufuatia uchunguzi wa kimaadili. Wamepatikana na hatia ya ukiukaji wa maswala mbalimbali kama vile kashfa ya dola milioni mbili malipo yasiyo rasmi ambazo zilikabidhiwa Patini mwaka 2011. Maafisa hao wawili wanasisitiza kutofanya makosa yoyote. Marufuku hiyo inaanza kutekelezwa mara moja. Rais huyo wa Fifa tangu mwaka 1998, Bwana Blatter, mwenye umri wa miaka 79, tayari ametangaza kujiondoa katika kinyanganyiro cha kumtafuta rais mpya wakati wa uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo mwezi Februari mwakani. Naye nahodha wa zamani wa Ufaransa Platini, mwenye umri wa miaka 60, na ambaye alionekana kama kiongozi wa baadaye wa shi...

KAMA ULIKUWA HAUJUI BASI JUA SASA.... DUNIANI WAWILI WAWILI>>unavyoona hawa wanafanana na Rooney, C. Ronaldo na Messi?

Image
Kwa upande wa Tanzania tumezoea kuona team ya XXL ya Clouds FM kuandaa show ya After School Bash  kwa ajili ya wanafunzi kuenjoy baada ya kupata muda wa kupumzika kutoka shule au chuo, na huwa kuna time watu waliofanana na mastaa hujitokeza kama sehemu ya burudani, sasa leo naomba nikusogezee hawa jamaa wanaotajwa kufanana na mastaa wa soka. 1- Cristiano Ronaldo anafananishwa na  Gokmen Akdogan Gokmen Akdogan huyu ni mshikaji kutoka Uturuki anatajwa kufanana sana na Cristiano Ronaldo, jamaa ana umri wa miaka 23 na amekuwa akipiga pesa nyingi kutokana tu na kufananishwa na Ronaldo, wanasema amekuwa akisaini autographs na wakati mwingine kulipwa kwa kutokea kwenye matukio mbalimbali. Kutoka kushoto Gokmen Akdogan na Cristiano Ronaldo 2- Wayne Rooney anafananishwa na  Aaron Ashmore Kama umepata bahati ya kuangalia  Warehouse na  Smallville kuna jamaa anaitwa  Aaron Ashmore anafanishw...