Mourinho akaribia kutua Old Trafford
Wamiliki wa Manchester United ndiyo wenye uamuzi wa mwisho wa kumtimua
Louis van Gaal baada ya Jose Mourinho kukubali kuwa kocha mpya wa miamba
hiyo ya Old Trafford.
Mazungumzo yamefanyika kati ya klabu na Mourinho, na Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Man United, Ed Woodward amefanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa mbadala wa Van Gaa anapatikana pindi utakapohitajika.
Kilichobaki sasa ni kwa familia ya Glazer kuamua kufanya mabadiliko hayo, na malumbano yaliyopo ni kumtimua Van Gaal sasa au kumpa nafasi ya mchezo ujao wa Jumamosi dhidi ya Stoke.
Bodi ya Old Trafford imekuwa katika majadiliano ya kumtimua Mholanzi huyo, ambaye alionekana kama chaguo la kwanza baada ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson, ambaye alishauri aitwe David Moyes.
Lakini kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Norwich Jumamosi kilikuwa cha tatu mfululizo kwa miamba hiyo ya Old Trafford na wasiwasi ni kwamba timu imekosa ari tena.
Kumaliza ligi katika nafasi ya nne na kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya ni mipango ya kati inayotegemewa na miamba hiyo baada ya kumsaidia Van Gaal kuwa na timu nzuri kwa kumpa Pauni 300 milioni tangu alipowasili.
Baada ya kushuka hadi nafasi ya tano, kengele ya hatari imeanza kulia ikiashiria kwamba kuna kitu kinatakiwa kufanyika ili kuepuka kutumia msimu mwingine bila mashindano ya Ulaya.
Kumekuwa na nafasi nyingine ya kufanya mabadiliko baada ya kuwapo kwa kocha mwingine wa kiwango cha juu (Mourinho) ikiwa watalazimika kumtimua Van Gaal. Woodward amefanya kazi ya ziada kuhakikisha kwamba Mourinho anakuwa tayari muda wowote kuichukua timu hiyo, na sasa suala hilo lipo mikononi mwa Avram na Joel Glazer kutoa ruhusa.

Comments
Post a Comment