Posts

Showing posts with the label SIASA KITAIFA

Baada ya Tarehe ya Uchaguzi Zanzibar Kutangazwa..CUF Watoa Msimamo Wao

Image
Kufuatia tangazo jengine la kihuni lisilozingatia Katiba wala Sheria la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha kutangaza tarehe 20 Machi, 2016 kwamba ni siku ya kile anachokiita uchaguzi wa marudio Zanzibar, Chama Cha Wananchi (CUF) kimeitisha vikao vya juu vya kitaifa vya Chama ili kujadili suala hilo na kutoa msimamo rasmi wa Chama. Kamati ya Utendaji ya Taifa itakutana Jumatano, tarehe 27 Januari, 2016 na kufuatiwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa litakalokutana Alkhamis, tarehe 28 Januari, 2016. Vikao hivyo vitafanyika Ofisi Kuu ya Chama, mjini Dar es Salaam. Chama kinatoa wito na kuwanasihi Wazanzibari wote waliochoshwa na utawala wa kibabe na wa kidikteta wa CCM na ambao walikikataa chama hicho kwa kishindo tarehe 25 Oktoba, 2015 kuendelea kutunza amani na kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu na kusubiri maamuzi ya chama chao wanachokiamini. HAKI SAWA KWA WOTE ISMAIL JUSSA KAIMU MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO

Kasi Ya Rais Magufuli Itaviua Vyama Vya Upinzani Hapa Nchini || Ni Kauli Ya Nape Nnauye:

Image
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Pichani, Nape Nnauye amesema kasi ya utendaji kazi ya Rais John Magufuli inaweza kuua uwepo wa vyama vya upinzani nchini. Hata hivyo alisema kuwa hangependa upinzani ufe kwa vile hiyo pia itakuwa imeua demokrasia nchini na kudai kuwa lengo la kuanzisha vyama vya siasa haikuwa kuviua bali ni kuviona vikiendelea kuwepo. Kauli hiyo ilitolewa juzi na Katibu huyo wakati alipokuwa akikagua maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe ya miaka 39 ya CCM ambayo kilele chake kimepangwa kufanyika mkoani hapa Februari 6, mwaka huu badala ya Februari 5 iliyozoeleka. Alisema kuwa chama kimelazimika kubadili tarehe ya kilele ili kuwawezesha wananchi kushiriki ipasavyo maadhimisho hayo kwa kufanya kazi badala ya kuwa na sherehe mbalimbali. “Maadhimisho ya safari hii ni tofauti na ya miaka mingine. Safari hii wananchi watatakiwa kushiriki zaidi kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo. Kauli mbiu yetu ni ‘Sasa kazi’ h...

UKAWA wasusia Kamati za Bunge Na Kugomea Uchaguzi......... Zitto Kabwe awaponda wao na Serikali, Awafananisha na 'Manyumbu'.

Image
Wakati vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge vikitarajiwa kuanza leo kwa uteuzi wa wajumbe, wabunge wa upinzani tayari wameanza kwa kumtikisa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai, baada ya kususia uchaguzi wa wenyeviti wa kamati hizo. Dalili za mgawanyiko kwenye kamati hizo zilianza kuonekana juzi, baada ya wabunge hao wa Kambi ya Upinzani kufanya kikao na kuweka msimamo wa kutaka kushirikishwa kwenye uteuzi wa wajumbe. Kambi ya Upinzani ilisema inataka kushirikishwa katika hatua hiyo ikidai kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM), imekuwa ikiwapangia watu wa kuongoza kamati zinazosimamia mapato ya serikali ambazo kikanuni zipo chini yao. Viongozi hao wa kambi ya upinzani walidai kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakipangiwa watu wa kuongoza Kamati ya Hesabu za Serikali za (PAC) na ile ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), ambazo kikanuni zinatakiwa kuongozwa na upinzani. Baada ya Ofisi ya Bunge kutangaza majina ya wajumbe wa kamati, Kambi ya Upinzani...

Mahakama Kuu Yafutilia Mbali Kesi Ya Kupinga Ushindi Wa Tundu Lissu

Image
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dodoma imefutilia mbali kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Jonathan Njau kupinga ushindi wa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu (CHADEMA). Katika madai yake ya msingi, Njau alikuwa akipinga matokeo na kutaka kura kuhesabiwa upya. Shauri hilo lilikuwa mbele ya Jaji Berkel Sehel ambapo mgombea wa ubunge kupitia chama cha Mapinduzi CCM Jonathan Njau alishindwa kwenye uchaguzi kwenye jimbo hilo mwaka 2010 na 2015. Njau Aliwasilisha ombi mahakamani la kutaka kesi hiyo kufutwa kwani hana haja ya kuendelea na shauri hilo. Awali mlalamikaji aliwahi kupeleka mahakamani mara mbili maombi ya ombi la kusamehewa kwa gharama za kesi kiasi cha milioni 15 lakini maombi hayo yalitupwa Lisu amesema Mahakama kuu ilishatamka mwaka 2010 kuwa kesi za uchaguzi si za kuendea kwa papara bila umakini wowote.

Waziri Mkuu Mstaafu ,Mizengo Pinda Awafunda Wabunge Wa CCM.....Awataka Kujenga Hoja Vizuri Ili Kuwakabili Wabunge Wa Upinzani

Image
WAZIRI Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda amewataka wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kujenga hoja vizuri katika Bunge linalotarajia kuanza vikao vyake wiki ijayo mjini Dodoma, kwa kuwa wabunge wa vyama vya upinzani wameongezeka bungeni. Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Pinda, baada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Leticia Nyerere, aliyefariki akiwa Maryland nchini Marekani akipatiwa matibabu. Akizungumzia Bunge la sasa, Pinda aliwashauri wabunge wanaounda Bunge hilo ambao wengi wao ni vijana, kuzingatia maslahi ya taifa na sio itikadi za vyama vyao na kuwasisitiza wabunge wa CCM, kujipanga na kwenda na hoja. “Kila upande ujiandae kwenye kuwasilisha hoja, kuna ongezeko la wabunge wa upinzani, sasa wabunge wa CCM ni lazima nao wajipange na kujenga hoja vizuri,” alisema Pinda.  Alisema kwa mtazamo wake, Bunge ni zuri na sio la mivutano kwa kuwa kila mmoja amejipanga kuwasilisha hoja zitakazomgusa mwananchi kwa lengo la kumsaidia....

Mkuu wa Oganaizesheni wa NCCR-Mageuzi Amtaka LOWASSA Ajieleze Kama Ataendelea Kubaki CHADEMA Iwapo Jina lake Litaenguliwa Mbio za Urais 2020

Image
Kufuatia  kauli ya aliyekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwavuli wa Ukawa, Edward Lowassa ya kugombea tena urais mwaka 2020, Mkuu wa Oganaizesheni wa NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura amemhoji Lowassa kama atakuwa tayari kuendelea kutumikia Ukawa kama jina lake halitapendekezwa kugombea nafasi hiyo. Sungura amesema kauli hiyo ya Lowassa kupambana tena katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2020 kunategemea maamuzi ya chama kupitisha jina lake. “Nimemsikia Lowassa anasema kuwa anajiandaa kupambana na Rais John Magufuli mwaka 2020, lakini je, yuko tayari kuheshimu maamuzi ya chama kwa maslahi ya wakati huo?” Alihoji Sungura. Sungura alisema mwaka jana jina la Lowassa lilipochujwa kwenye wagombea urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) alijiondoa na kuhamia Chadema. “Je, atakuwa tayari kuheshimu maamuzi ya chama pale ambapo jina lake halitapitishwa kugombea urais Chadema au atahamia chama chak...

Siri kuvunjika mazungumzo ya mwafaka Zanzibzr Yabainika Soma Hapa

Image
Aliyekuwa mgombea urais wa CUF, Maalim Seif Sharif. Wakati hatua ya aliyekuwa mgombea urais wa CUF, Maalim Seif Sharif, ya kujitoa kwenye mazungumzo ya maridhiano yaliyokuwa yakiendelea visiwani Zanzibar ikiwa imeacha mshangao kwa wananchi, Nipashe imebaini siri ya kujiondoa kwake.   Maalim Seif alijiondoa katika mazungumzo ya kutafuta maridhiano ya muafaka katika kamati iliyowajumuisha Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Dk. Salmin Amour Juma, Amani Abeid Karume na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.   Katika kamati hiyo iliyowahi kukutana mara tisa kwa nyakati tofauti ili kutatua mgogoro huo bila ya kufikiana muafaka, inaelezwa kuwa kulikuwa na mvutano mkubwa kati ya wastaafu hao na Maalim Seif.   Kutopatikana kwa muafaka wa vikao hivyo, Januari 11, mwaka huu, Maalim Seif alitoa sababu kadhaa za kutotaka uchaguzi huo kurudiwa huku akimwomba Rais Dk. J...

HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA VYAMA VYA UPINZANII..... UKAWA KUUNDA CHAMA KIMOJA CHA SIASA CHENYE NGUVU ZAIDI,

Image
DAR24 DAR24 DAR24 UMEISIKIA HII KUTOKA UKAWA:::MPANGO WA KUUNDA CHAMA KIMOJA CHA SIASA WAIVA,SOMA HAPA ZAIDI. - See more at: http://www.mambomsetotz.com/2015/12/umeisikia-hii-kutoka-ukawampango-wa.html#sthash.AYgAptJp.ObXC0EBS.dpuf UMEISIKIA HII KUTOKA UKAWA:::MPANGO WA KUUNDA CHAMA KIMOJA CHA SIASA WAIVA,SOMA HAPA ZAIDI. - See more at: http://www.mambomsetotz.com/2015/12/umeisikia-hii-kutoka-ukawampango-wa.html#sthash.AYgAptJp.ObXC0EBS.dpuf UMEISIKIA HII KUTOKA UKAWA:::MPANGO WA KUUNDA CHAMA KIMOJA CHA SIASA WAIVA,SOMA HAPA ZAIDI. - See more at: http://www.mambomsetotz.com/2015/12/umeisikia-hii-kutoka-ukawampango-wa.html#sthash.AYgAptJp.ObXC0EBS.dpuf UMEISIKIA HII KUTOKA UKAWA:::MPANGO WA KUUNDA CHAMA KIMOJA CHA SIASA WAIVA,SOMA HAPA ZAIDI. - See more at: http://www.mambomsetotz.com/2015/12/umeisikia-hii-kutoka-ukawampango-wa.html#sthash.AYgAptJp.ObXC0EBS.dpuf