Posts

Showing posts with the label BUNGENI

BUNGE LA WAKA MOTO>>> WABUNGE WA UPINZANI WAGOMA KUTOKA NJEEE>>

Image
Kinenuka bungeni hivi.....wapizani waliambiwa watoke nche waka goma mw Chenge akaamuru police waingie nawametolewa nche kama kawaida ccm wamebaki wanaendelea kubwabwaja utumbo wao...... V KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA CHINII>>>>>

Matukio Mbalimbali Ya Bunge Leo Mjini Dodoma

Image
Matukio Mbalimbali Ya Bunge Leo Mjini Dodoma Waziri Mkuu, Kassim Majalliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama Buneni mjini Dodoma Januari 27, 2016. Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia)  akimwapisha Waziri wa Elimu , Sayansi, Tekinolojia na Mafunzo ya Ufundi Joyce  Ndarichako, bungeni mjini Dodoma Januari 27, 2016. Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii,na Michezo  Nape Nnauye akitoa  kauli Bungeni mjini Dodoma Januari 27, 2016.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, Bungeni mjini Dodoma January 27, 2016. Mwenyekiti wa Bunge, Mtemi Andrew Chenge  akiongoza kikao cha Bunge mjini Dodoma Januari 27, 2016.
Image
Andrew Chenge Achaguliwa Kuwa Mwenyekiti wa Bunge.....Asema Suala La Escrow Likirudi Bungeni Atakaa Pembeni  MBUNGE wa Bariadi, Andrew Chenge na wabunge wawili wa Viti Maalumu, Dk Mary Mwanjelwa na Najma Giga, wamechaguliwa kuwa Wenyeviti wa Bunge kwa kipindi cha miaka miwili na nusu. Uchaguzi huo ulifanyika jana baada ya majina yao kupendekezwa na Kamati ya Uongozi na kuyawasilisha bungeni kwa ajili ya uchaguzi.  Katika uchaguzi huo, uliotanguliwa na wabunge hao kujieleza mbele ya wenzao na kuulizwa maswali, sakata la Tegeta Escrow liliibuka baada ya Chenge kujieleza. “Katika Bunge lililopita, chama chako na wabunge walikuwajibisha kwa kashfa ya Escrow, je, siku ukiliongoza Bunge na hoja ikarudi ndani uko tayari kuisimamia,” Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe (Chadema) alimuuliza Chenge. Akijibu swali hilo, Chenge alisema Bunge linaongozwa na Kanuni na itakapokuja mbele ya Bunge au kwenye Kamati, ikaonekana kuna maslahi ...

breaking news>>> Zitto Kabwe Awasha Moto Bungeni

Hoja ya gharama ni hoja dhaifu sana katika kuzuia mikutano ya Bunge kurushwa 'live'. Demokrasia ni gharama Posted by Zitto Kabwe on  Wednesday, January 27, 2016

Zitto Kabwe na Saed Kubenea Kukutana Uso Kwa Uso Kamati Ya Huduma za Maendeleo ya Jamii

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ametangaza kamati za Bunge na majina ya wabunge waliochaguliwa katika kamati hizo kwa mujibu wa sheria. Sura za wabunge wa zamani zimechanganyika na sura mpya katika kamati hizo ambapo Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT) na Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea (CHADEMA) ni miongoni mwa wanaounda kamati ya huduma za maendeleo ya jamii. Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula (CCM), Naghejwa Kaboyoka Same mashariki (CHADEMA)Livingstone Lusinde Mtera (CCM) wameteuliwa kujumuika katika kamati ya Hesabu za serikali PAC. Kamati nyingine ni pamoja na Kamati ya Uongozozi ikiwa na Spika Job Ndugai ambaye ni Mbunge wa Kongwa (CCM), Freeman Mbowe Hai (CHADEMA) George Masaju ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wengineo. Kamati ya sheria ndogo waliopata nafasi ni pamoja na Halima Mdee Kawe (CHADEMA),Abdalah Mtolea Temeke (CUF) ,Tundu Lissu Singida Mashariki (CHADEMA),Ridhiwani Kikwete Chalinze (CCM). Baadhi ya wana...

Kubenea Aibua Ufisadi wa Billion 1.2 Kupitia Ufuaji wa Majoho ya Madiwani

Image
MBUNGE wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea ameibua ufisadi wa Shilingi bil. 1.2 kwa mwaka katika Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam unaofanywa kupitia ufuaji wa majoho ya madiwani. Kubenea amesema hayo Stendi Kuu ya mabasi yaendayo mikoani alipofanya ziara ya siku moja kutembelea soko la Urafiki maarufu kama Mahakama ya ndizi, soko la Mabibo na kuhitimisha ziara yake katika Stendi za Ubungo na Simu 2000 “Baada ya kufanya uchunguzi tumebaini kuwa mradi huo wa ufuaji majoho kabla ya madiwani kufanya kikao unaotumia shilingi bilioni 1.2 hivyo basi Halmashauri ya Manispaa itakayokuwa chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) tukianza kazi tutaufuta,” alisema Kubenea. Aliongeza kuwa kufutwa kwa mradi huo kutafanywa mara moja baada ya Ukawa kupata Meya wa Manispaa na Jiji kutokana na ukweli kwamba wana Halmashauri mbili kati ya tatu hivyo zitawawezesha kumpata Naibu Meya katika Chama Cha Wananchi (CUF) na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Kubenea alisema jambo jingin...

Bunge Kuondoa Ajira za Kudumu Serikalini.....Kudumu Kwa Ajira Ya Mfanyakazi Kutategemea Juhudi Zake Kazin

Image
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litafanyia mabadiliko makubwa sheria za utumishi wa umma kwa kuondoa ajira za kudumu serikalini, ili kuwezesha mabadiliko yaliyokusudiwa na Rais Dk. John Magufuli. Katika mabadiliko hayo, mfumo sasa wa ajira za serikali kuwa za kudumu utabadilishwa na badala yake, kudumu kwa ajira ya mfanyakazi kutategemea juhudi na bidii yake kazini, ili kuondoa uzembe uliodumu miaka nenda miaka rudi, katika sekta ya umma. Akizungumza katika mahoajino binafsi na gazeti la  Raia Mwema, mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, alisema baadhi ya sheria za kazi zinawafanya baadhi ya watumishi wa umma kuwa wazembe. “ Kwa mfano katika serikali ya sasa mfanyakazi mzembe kabisa kabisa hata waziri kumfukuza kazi hawezi. Hata Katibu Mkuu hawezi mpaka afuate mlolongo mrefu na hatua nyingi sana, yaani kazi ni guarantee (uhakika) katika nchi yetu ni permanent and pensionable (ya kudumu na ina pe...

Uteuzi wa Waziri Mkuu: Spika Job Ndugai Kukabidhiwa Bahasha ya Jina La Waziri Mkuu Kesho.....Ijumaa Kuapishwa

Image
Baada ya wabunge kumchagua Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai kuwa Spika wa Bunge la 11 jana, anayesubiriwa ni Waziri Mkuu mpya ambaye anatarajiwa kujulikana kesho Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya Bunge, kesho Alhamisi, Bunge litapokea na kuthibitisha kwa kupiga kura jina la Waziri Mkuu wa 11 wa Tanzania ambalo Dk Magufuli atakuwa ameliwasilisha kwa Spika Job Ndugai. Baada ya kutoa  jina la Waziri Mkuu, Dk Magufuli anatarajia kulihutubia Bunge, Ijumaa saa kumi baada ya kuwa amemwapisha Waziri Mkuu asubuhi. Hotuba yake ya Kwanza Bungeni  itakuwa dira ya utawala wake kwa miaka mitano ijayo akiwa na kauli Mbiu ya Hapa kazi tu.

UKAWA Kumpokea Rais Magufuli Bungeni Kwa Staili Mpya

Image
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umesema utakuja na stahili mpya wakati  Rais Dk. John Magufuli, atakapokwenda  kuzindua na kuhutubia Bunge Novemba 20, mwaka huu. Umesema staili watakayoitumia ni tofauti na ile waliyoitumia wakati Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, alipozindua Bunge la 10 mwaka 2010 ya kutoka nje ya ukumbi kuonyesha kutotambua serikali yake. Akizungumza na mtandao huu katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana, aliyekuwa Mnadhimu wa Bunge la 10 Kambi la Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, alisema safari hii hawatatoka nje ya ukumbi wa Bunge  hata kama hawamkubali Rais Magufuli, kwa kuwa ni wajibu wao kushiriki vikao vya chombo hicho cha kuwakilisha wananchi. “Sisi ni wabunge, tumo humu kwa ridhaa ya wananchi, tuna haki ya kuingia bungeni, hivyo siku hiyo tutaingia lakini kitakachotokea tutajua siku hiyo, bali haitakuwa kama walivyotuzoea tunatoka nje,” alisema na kuongeza: “Subira yavuta heri, bado siku tatu tu, Watanzania watajua msimam...

Bunge Laanza kwa Spidi: Nape Apigwa Dongo, Aambiwa Anasumbuliwa Na Utoto

Image
Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeanza jana mjini Dodoma na moto ambao wengi waliutabiri huku harufu ya ushabiki wa vyama ikitawala. Katika zoezi la kumtafuta Spika wa Bunge hilo lililotanguliwa na maswali na majibu kwa wagombea nane waliojitokeza, Mgombea Uspika kupitia Chadema, Goodluck ole Medeye alikwaruzana kimtazamo na mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye. Swali la Nape lililokuwa kati ya maswali matatu aliyoulizwa Ole Medeye lilionekana kumuudhi mgombea huyo. Nape alimtaka Ole aeleze kama ameacha tabia ya ubaguzi kwa madai kuwa Godbless Lema aliwahi kumtuhumu kuwa ni mbaguzi. Ingawa Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo, Andrew Chenge alikataa swali hilo lisijibiwe akieleza kuwa halikuwa swali, Ole Medeye alihitimisha kwa kumueleza Nape alichokuwa nacho moyoni ingawa hakumtaja jina. “Kuna mbunge hapa aliniuliza swali ambalo kwa lugha za kibunge tunaliita ni swali la kuudhi. Mbunge huyo nimemsamehe, sina chuki naye kwa sababu najua kinachomsumbua ni u...