Jinsi Vyakula Vinavyosababisha Magonjwa
Jinsi Vyakula Vinavyosababisha Magonjwa Jarida la Emerging Infectious Diseases linasema kwamba zaidi ya magonjwa 200 yanaweza kusababishwa na chakula. Hata hivyo, vijidudu vinavyosababisha magonjwa hayo yote si vingi sana. Huenda takwimu zifuatazo zinaweza kufanya mtu afikiri hivyo. Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), kila mwaka watu milioni 130 hivi katika Eneo la WHO huko Ulaya wanaambukizwa magonjwa yanayosababishwa na chakula. Katika mwaka wa 1998, zaidi ya watu 100,000 nchini Uingereza walikuwa wagonjwa kwa sababu ya kula chakula kibaya, na 200 kati yao walikufa. Inakadiriwa kwamba kila mwaka watu milioni 76 hivi wanapata magonjwa yanayosababishwa na chakula huko Marekani, na 325,000 kati yao hulazwa hospitalini, na 5,000 hufa. Si rahisi kujua hesabu kamili ya ulimwenguni pote. Hata hivyo, shirika la WHO linaripoti kwamba watu milioni 2.2 hivi walikufa kutokana na magonjwa ya kuharisha katika mwaka wa 1998, na milioni 1.8 kati yao walikuwa wat...