Posts

Showing posts with the label DIAMOND PLATINUMZ

DIAMOND AKANUSHA KUPEWA MILIONI 500 NA LOWASSA ILI AMPIGIE KAMPENI....ASEMA TAARIFA HIZO ZINALENGO LA KUMCHAFUA LOWASSA

Image
Meneja  wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’, Babu Tale, amesema hawajawahi kupewa kiasi cha fedha Sh mil 500 na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ili wampigie kampeni za urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).   Akizungumza na Mpekuzi, Babu Tale alisema watakuwa wehu kukataa fedha nyingi kiasi hicho wakati wenyewe wanafanya muziki ili kupata fedha, lakini ukweli ni kwamba hawajapewa kitu chochote.   Alisema hata hivyo Diamond yupo tayari kumfanyia kampeni mgombea yeyote atakayetangazwa kuiwakilisha CCM.    “Kama kweli tungekataa fedha hizo hata Mwenyezi Mungu angetulaani, ila naamini taarifa hizo zitakuwa zinasambazwa na wapinzani wa kisiasa wa kiongozi huyo kwa  lengo la kumchafua, hajawahi kutupa ofa hiyo,” alisema Babu Tale.   Meneja huyo alitoa ufafanuzi huo baada ya hivi karibuni kuzagaa kwa taarifa ambazo si za kweli, kwamba walipokea kiasi hicho ili kumpigia kampeni Lowassa.

Mama Wema Sepetu Afurahia Ujauzito wa Zari, Aombea Zari Azidi Kumganda Diamond..Kisa na Mkasa Huu Hapa

Image
Udaku Special Blog: SIKU chache baada ya kuvuja kwa picha zinazomuonesha mpenzi wa sasa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa na kitumbo kinachoashiria kukua kwa ujauzito, mama mzazi wa zilipendwa wa Diamond, Wema Sepetu ‘Madam’, Mariam Sepetu amefunguka kuwa amefurahia tukio hilo. Mzazi huyo ambaye ni fundi wa kuzungumza, alisema tukio hilo limemfurahisha kwani anaamini ndoto za Diamond kurudiana na binti yake zitakuwa zimeyeyuka rasmi kama alivyokuwa akimuomba Mungu siku zote. Kuonesha kwamba amefurahishwa na kitendo hicho, alimtaka Zari aendelee kumpenda Diamond, amgande kila idara ili isije kutokea akarudi kwa binti yake ambaye walimwagana mwishoni mwa mwaka jana. “Yaani kama inawezekana naomba sana huyo Zari azidi kumganda Diamond, asimpe muda wa kugeuka nyuma kabisa ili mambo mengine yaendelee kwa sababu uhusiano wa Diamond na mwanangu haukuwa na baraka zangu,” alisema mama Wema. Mama Sepetu aliongeza kuwa, hana maana ya kumchagulia mchum...