Posts

Showing posts with the label HABARI

Simon Msuva: Kiba anaitendea haki Tanzania

Image
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva ambaye msimu huu ameifungia klabu yake jumla ya mabao 14 amefunguka kwamba, msanii Alikiba anaitendea haki nchi yake ya Tanzania kwa kazi ya muziki ambapo amekuwa akifanya kazi bora zinazoleta sifa kwa nchi. Msuva amesema hayo leo kupitia kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kusema yeye anamkubali sana msanii huyo kutokana na uwezo wake kimuziki na namna anavyoweza kuimba vizuri kila apatapo nafasi. "Kwanza naupenda sana ule wimbo wa wale jamaa wa Kenya wameshirikisha Alikiba 'Unconditionally Bae', naukubali ule wimbo sababu watu wamepangilia sana kazi yao mle ndani na unayasikia kabisa, nimependa mavazi ya mule jinsi walivyovaa ni mavazi fulani ambayo yanawakilisha Afrika japo hata watu wa Ulaya wanavaa lakini naona Afrika watu wanapenda sana kuvaa vile" alisema Msuva Msuva aliendelea kutoa ufafanuzi juu ya wimbo huo na uwezo wa Alikiba "Ukisikiliza ule wimbo unaona jinsi ambavyo Alikiba amefanya vi...

#BREAKING: Wanafunzi wengine watatu wamepoteza maisha leo Geita

Image
Nimeipata hii taarifa kutoka mkoani Geita ikieleza kumetokea ajali ya Mtumbwi ambao ulibeba wanafunzi wa shule ya Ludegea ambapo wanafunzi watatu wamepoteza maisha baada ya kuzama na wengine 21 wamenusurika. Imeelezwa kuwa wanafunzi hao walikuwa njiani kuelekea shuleni wakati ajali ya kuzama mtumbwi huo ilipotokea.

Binti wa miaka 15 abakwa na vijana wanne Jijini Mwanza

Image
    Watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi huku mwingine mmoja akiendelea kutafutwa kwa tuhuma za kumbaka binti mmoja mwenye umri wa miaka 15 wilayani Ilemela, mkoani Mwanza. Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amesema kwamba tukio hilo limetokea tarehe 21/05/2017 majira ya saa moja kamili jioni katika maeneo ya mamlaka ya pamba, kata ya Kirumba ambapo inadaiwa kuwa binti huyo ambaye pia ni mkazi wa Kirumba alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtuhumiwa aliyejulikana kwa jina moja la Phili na walipanga wakutane katika maeneo hayo. Inasemekana kuwa binti huyo alikutana na mpenzi wake mahali hapo kisha walikwenda sehemu yenye jumba bovu kuzungumza, wakiwa kwenye eneo hilo ghafla walitokea vijana wengine watatu wakishirikiana na Phili na kuanza kumfanyia ukatili kwa kumbaka. Inasemekana kuwa wakati wakiendelea na ukatili huo binti alipiga yowe akiomba msaada kutoka kwa wananchi, wananchi walifika eneo la tukio ...

Kujiuzulu kwa Waiguru kulivyopisha mabadiliko

Image
Waziri wa Ugatuzi Bi Anne Waiguru muda mfupi kabla ya kujiuzulu Novemba 21, 2015. Picha/WILLIAM OERI  Na CHARLES WASONGA Imepakiwa - Sunday, November 29  2015 at  14:53 Kwa Mukhtasari Kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Ugatuzi  Bi Anne Waiguru ndiko kuliwachochea Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto kuafikiana haraka kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri Jumanne baada ya shughuli kucheleweshwa kwa miaka kadhaa, wabunge na wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema. KUJIUZULU kwa aliyekuwa Waziri wa Ugatuzi  Bi Anne Waiguru ndiko kuliwachochea Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto kuafikiana haraka kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri Jumanne baada ya shughuli kucheleweshwa kwa miaka kadhaa, wabunge na wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema. Kuondoka kwa waziri huyo kuliacha baraza hilo na mawaziri 13  peke...

Siasa » Hili la Wakuu wa Mikoa/Wilaya Kufuta Likizo ni Kuweka Watu Vizuizini ni Ukiukwaji wa Sheria!

Image
Hili la Wakuu wa Mikoa/Wilaya Kufuta Likizo ni Kuweka Watu Vizuizini ni Ukiukwaji wa Sheria!     Siungi mkono na sitothubutu kuunga mkono matamko ya wakuu wa mikoa ya Tanga na Kilimanjaro kufuta likizo za watumishi wa umma kwa mwezi huu wa December bila kutolewa ufafanuzi wa kisheria! Hizi ni dalili za utawala wa kimabavu na usiotumia weledi na maadili ya kazi! Likizo za watumishi wote wa umma zipo kwa mujibu wa sheria! Mfanyakazi yeyote yule wa umma aliyeajiriwa na anayelipa kodi serikalini ana haki ya msingi kabisa ya kupata likizo ya siku 28 kwa kila mwaka wa utumishi! Hata waalimu huwa hawaendi likizo pale ambapo wanafunzi wamefunga shule! Wao huwa na likizo zao ambazo zipo kwa mujibu wa sheria! Mkuu wa wilaya kuweka watumishi wa umma kifungoni bila kuwa na maelezo yoyote ya kuridhisha ni dalili za utawala wa kimabavu hatuongozi nchi kwa "Presidential decree" Kiasi kwamba kila kiongozi anaweza kufanya maamuzi kwa kutamka tu na kisha akawa haojiwi! Kumuweka ...

John Magufuli » Je Kasi ya Magufuli na Watendaji Wake Ndio Mwanzo wa Udikteta? Ama ni Kasi Inayotakiwa Katika Taifa Hili ?

Image
       Je Kasi ya Magufuli na Watendaji Wake Ndio Mwanzo wa Udikteta? Ama ni Kasi Inayotakiwa Katika Taifa Hili ? Mwalimu Nyerere once a time alisema kama nigetaka kuwa dicteta ningeweza. hivi sasa watanzania tumepata upofu wala hatuoni tena. nimewahi kusema kwenye post zangu kuwa IPO siku watanzania watamkumbuka Rais Kikwete. kwanini niseme ivo, twende pamoja na kama unamatongotongo kanawe,na kama umemeza viroba kaa mbali na hii post,only great thinkers. 1. VITISHO NA HOFU ukubali au ukatae magufuli sasa anaogopwa na amejaza hofu wananchi haswa wafanyakazi na wafanyabiashara. kumbekeni Adolph Hitler alishinda uchaguzi wala hakupindua serikali pia alipata public sympathy hata pale alipokesea. tazama sasa hata hii post kuna watu watakosoa bila kujali relevance yake. 2. KUVUNJWA KWA HAKI ZA BINADAMU. hivi sasa unaweza kuweka polisi bila kushtakiwa mfano. hivi jeuri ya Paul Makonda yakumweka MTU kizuizini bila kumpeleka mahakamani ni uvunjaji wa haki...

Viongozi Waliojiuzulu Chadema Warejea Tena

Image
Viongozi wa Chadema Mkoa wa Rukwa waliotangaza kujiuzulu nyadhifa zao ndani ya chama hicho hivi karibuni, wamesitisha uamuzi wao na kurejea madarakani. Mratibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Frank Mwaisumbe alisema hayo juzi wakati akizungumza na mwandishi w etu  kwa njia ya simu kutoka mkoani Mbeya. Mwaisumbe alisema wamekubaliana na viongozi hao kurejea katika nyadhifa zao za kisiasa ndani ya chama hicho. Alisema kikao baina ya viongozi wa Chadema wa kanda hiyo na waliotangaza kujiuzulu kilidumu kwa zaidi ya saa 11 juzi na kufikia uamuzi wa kurejea madarakani kwa viongozi hao. Akizungumzia sababu za kujiuzulu kwa viongozi hao ambazo ni kutolipwa fedha mawakala wa wagombea wa chama hicho mkoa na kutoridhishwa na uteuzi wa mgombea ubunge wa viti maalumu, Aida Kenan, alidai zina mashiko lakini kabla ya kutangaza katika vyombo vya habari kuachia ngazi walipaswa kuwasiliana na uongozi wa juu wa chama. Aliongeza kuwa, mathalan katika suala la mawakala kulikuwa na...

IKULU: Katibu Wa Wizara ambaye ni Goigoi Ajiondoe Mapema

Image
Joto la utawala wa Rais John Magufuli limebadili utendaji kazi wa makatibu wakuu wa wizara mbalimbali waliozoea kukaa ofisini na sasa wanafanya kazi nje ya ofisi na kusikiliza kero za wananchi kwenye maeneo yao . Wakati hilo likifanyika, Ikulu jijini Dar es Salaam imesema katibu mkuu au mtumishi yeyote wa umma atakayeshindwa kwenda na kasi na mabadiliko ya utendaji kazi katika serikali ya awamu ya tano ajiondoe. Tamko hilo linalotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alipohojiwa jana  kuhusu kutokuwapo kwa makatibu wakuu wa wizara kadhaa kwenye ofisini zao wiki iliyopita.    Makatibu wakuu wa Wizara kadhaa wamelazimika kuzifunga ofisi zao na kuelekea mikoani ku sikiliza kero za wananchi. Hali ya viongozi hao kuhama jiji na kwenda mikoani imeleta mabadiliko ya utendaji kazi wao baada ya miaka ya nyuma kuzoeleka kutumia muda mwingi ofisini na kuacha kazi za nje kufanywa na waziri, naibu au watendaji wengine. Baadhi ya wizara ambazo zilitembelewa ...

Siasa » Balozi zatakiwa Kujipanga Kuiwakilisha Tanzania Nchi za Nje

Image
Kufuatia agizo la Rais John Magufuli alilotoa hivi karibuni la kusitisha safari za nje kwa wizara, idara na taasisi za serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imeanza kutekeleza kwa kutoa maelekezo kwa Balozi zake za nje. Wizara hiyo imezielekeza Balozi zote zilizopo maeneo mbalimbali duniani kujipanga ili kushiriki kikamilifu katika kuiwakilisha serikali kwenye mikutano yote ya kimataifa na kikanda inayofanyika katika maeneo yao ya uwakilishi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam na wizara hiyo, imeeleza Tanzania ina Balozi 35 zikiwamo bazozi ndogo tatu, vituo viwili vya biashara na konseli za heshima 17 katika nchi mbalimbali. “Hizi zote zitahusika katika kuendeleza utekelezaji wa diplomasia yetu ya uchumi na uwakilishi wa maslahi ya nchi yetu,” ilieleza taarifa hiyo. Hadi sasa mikutano ambayo tayari imefanyika na Balozi zetu kuwakilisha ni pamoja na Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) unaoe...

» John Magufuli » Kasi ya Magufuli yazidi Kuwaweka Watendaji wa Serekali Roho Juu

Image
Katika kile kinachoonekana ni kutaka kwenda na kasi ya rais wa awamu ya tano, Dk. John Magufuli, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Rada kata ya Majohe, Jimbo la Ukonga, Abdallah Goma, amewatimua ofisini wajumbe watano wa mtaa na kuwataka waende mitaani kukusanya kero zinazowakabili  wananchi. Mwenyekiti huyo aliamua kuchukua hatua hiyo baada ya  wananchi kulalamikia tabia ya wajumbe  hao kuwadai  malipo  wakati  wanapokwenda kutaka huduma katika ofisi hiyo, ikiwamo kuandikiwa barua ya utambulisho benki. Goma aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam  jana kutokana na mvutano uliojitokeza  kati yake na wajumbe aliowatimua kugoma kutekeleza agizo lake na kususia vikao. Alisema  baada ya kuapishwa alipanga ratiba ya kila mjumbe kukaa ofisini kwa muda wa siku mbili, lengo likiwa ni kubaini tabia zao, hivyo katika kipindi hicho malalamiko ya lugha chafu, kudai malipo ya kuandika barua ya dhamana na utambulish...

Marehemu Mawazo alivyoagwa na wana-CHADEMA Mwanza leo.. (Picha) #RIP

Image
Taarifa iliyotolewa jana na viongozi wa CHADEMA Mwanza ilielekeza utaratibu wa siku tatu mfululizo mpaka mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Geita, Marehemu Alphonce Mawazo. Leo kuanzia asubuhi taratibu zilianza kwa kuutoa mwili wa Marehemu Hospitali, wakaelekea viwanja vya Furahisha vilivyopo katikati ya Mwanza kwa ajili ya shughuli za kumuaga marehemu ambapo viongozi mbalimbali wa CHADEMA wamewaongoza wanaCHADEMA waliokusanyika katika viwanja hivyo kumuaga marehemu. Hapa ninazo picha za tukio lote. Mzee Edward Lowassa Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe Mzee Frederick Sumaye Salum Mwalimu Mtoto wa marehemu Mawazo .

Marehemu Alphonce Mawazo Aagwa Rasmi Jijini Mwanza......Lowassa Atoa Tamko Zito Mbowe Aapa Kumfungulia Kesi ya Madai RPC -Mwanza

Image
A liyekuwa mgombea Urais wa Chadema, Edward lowassa, amelitaka jeshi la Polisi nchini kuwachukulia hatua wale wote wanadaiwa kumuua, aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo na kwamba kama hawatafanya hivyo, watachukua hatua wao wenyewe. Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni siku mbili sasa tangu Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, kutoa hukumu kwa chama hicho kikuu cha upinzani kumuaga na kumzika Marehemu Mawazo bila kuingiliwa na mtu yeyote. Marehemu Mawazo, alifariki Novemba 14 mwaka katika kijiji na kata ya Katoro, wilaya na Mkoa wa Geita kwa kukatwa mapanga na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa CCM. Lowassa ametoa kauli hiyo leo wakati akitoa salamu za rambirambi katika ibada ya kuaga mwili wa Mawazo kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza. Lowassa ambaye alikuwa mgombea wa Chadema na kuungwa mkono na vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) amesema polisi wasipochukua hatua kwa waliomuua marehemu Mawazo watajichukulia hatua wao. Amesema kuwa wat...

Waraka wa Kufuta Ada Elimu ya Sekondari ( Kidato cha 1 Hadi 4) na Michango yote Elimu ya Msingi

Image
Serikali imeamua kutoa elimu pasipo malipo kwa elimumsingi kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne,kuanzia mwaka wa masomo wa 2016.   Azima hii ya serikali ni katika kutekeleza sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ambayo ina lengo la kuhakikisha kwamba watoto wote wa Tanzania wanapata Elimu bila kikwazo ikiwemo ada au malipo. Katika kutekeleza maamuzi hayo,ada zote zilizokuwa zikilipwa kwa ajili ya elimu ya kidato cha kwanza hadi cha nne zimefutwa .Pia, waraka wa Elimu namba 8 wa mwaka 2011 kuhusu michango shuleni nao pia umefutwa. Aidha, mwongozo wa elimumsingi bila malipo unaandaliwa na utatumwa kwa wamiliki wa shule ifikapo au kabla ya tarehe 15 Disemba 2015. Waraka huu umeanza kutumika tarehe 21 Novemba 2015

Serikali Kudhibiti Uchapishaji wa Kalenda na Vitabu vya Kumbukumbu Katika Ofisi zote za Umma

Image
Katibu  M kuu K iongozi Balozi Ombeni Sefue ametoa ufafanizi wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John  Pombe Magufuli kuhusu kupunguza matumizi yasiyo ya lazima katika W izara,idara na T aasisi za serikali. Katika ufafanuzi huo,Balozi Sefue amemtaka kila M tendaji M kuu ama Afisa Masuhuli wa serikali kujiuliza mwenyewe ni kwa kiasi gani anatekeleza kwa vitendo nia y a Rais ya kuepuka matumizi yasiyo ya lazima "Rais ameonesha njia, sasa kwa wakati huu ni vema kila mtendaji mkuu wa serikali,ajiulize endapo Rais atafika katika eneo langu la kazi,ni kwa kiasi gani atakuta nimetekeleza maagizo yake?" Amesisitiza Balozi Sefue Kutokana na ufafanuzi huo, Blozi Sefue pia amezungumzia uchapishaji wa kalenda na vitabu vya kumbukumbu yani  "Diaries" akisema kila mtendaji mkuu wa Serikali ama Afisa Masuhuli apime mwenyewe kama ni lazima kutengeneza au kuchapisha kalenda na Diary? na kama ni lazima achapishe kwa kiasi gani? "Ni matumizi mab...

Mtandao wa Wauza Madawa ya Kulevya Waanza Kushughulikiwa..Mmoja Akamatwa Leo Mwenge Akiwa Dukani Kwake

Image
Mtandao wa Wauza Madawa ya Kulevya Waanza Kushughulikiwa..Mmoja Akamatwa Leo Mwenge Akiwa Dukani Kwake Siku kadhaa nyuma niliweka Uzi unaosema Hussein Mafisi analindwa na nani? Kwenye Uzi huo nililalamika ni nani anayemlinda Hussein Mafisi muuza madawa maarufu Mwenge. Leo muda wa saa 9 na dakika 45 amekamatwa. Gari tatu za Polisi zilifika Dukani kwake na kubeba mateja wote waliokuwepo na Hussein wenyewe.. Hii ni mara ya kwanza kukamatwa, daima hukamatwa mateja na yeye huachwa, lakini Leo kakamatwa. Nitasikitika Sana kama nitamkuta tena jioni akiendelea na biashara yake. Magufuli kata Hii network ya wauza unga.. Source: Nazijaz/Jamii Forums

Siasa » Kasi ya Rais Magufuli Yaibua Utata Kuhusu Home Shopping Centre Kufilisika

Image
Mwana masumbwi wa Marekani aitwaye Joe Louis aliwahi kusema, ''He can run, but he can't hide''. Kitendo cha Rais wa Tanzania na Waziri Mkuu wake, Majaliwa Kassim Majaliwa kuigusa kiutaratibu na kisheria Mamlaka ya Bandari na Mamlaka ya Mapato kimetoa picha kwa wachambuzi kuhusu kile ambacho kilikuwa kinafanyika kuhusu rushwa/ufisadi unaoendelea katika Mamlaka hizo. Kufilisika kiusanii kwa kampuni kama Home Shopping Centre wakati Uchaguzi Mkuu umebakiza wiki moja haikuwa ajabu kutokana na hali halisi ya utendaji wa mamlaka za nchi lakini kinachostaajabisha kwa sasa ni jinsi ambavyo mamlaka ya nchi imekuwa ikifahamu wakwepa kodi kuanzia wakuu wake mpaka waendesha gari la mizigo inayobeba makontena ambayo hajalipiwa ushuru. Nimeshangazwa kusikia taasisi ya Rais Magufuli imedadavua mpaka kufahamu idadi ya makontena ambayo yameingia mitaani bila kulipiwa ushuru. Mshangao huu umenifanya kuangalia nyuma na kugundua kuna kampuni ambayo ilifilisika ghafla bila mae...

Watumishi Wengine Watatu Wasimamishwa Kazi TRA

Image
SERIKALI imewasimamisha kazi watumishi watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao jana iliamriwa kwamba watahamishiwa mikoani. Watumishi hao ni Bw. Anangisye Mtafya, Bw. Nsajigwa Mwandengele na Bw. Robert Nyoni. Uamuzi huo umetolewa leo (Jumamosi, Novemba 28, 2015), na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ili kupisha uchunguzi zaidi wa tuhuma zinazowakabili.    Kama ilivyo kwa wenzao sita waliosimamishwa kazi jana (akiwemo aliyekuwa Kamishna Mkuu), nao pia hawaruhusiwi kusafiri kwenda nje ya nchi hadi uchunguzi utakapokamilika.  “Kazi ya kuwachunguza ilianza jana ileile na sasa, tumeona hawa watu wanapaswa kuwa nje ya utumishi ili kupisha uchunguzi ufanyike kwa uhuru zaidi,” alisema Waziri Mkuu. Pia Waziri Mkuu amemuagiza Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dkt. Philip Mpango atekeleze maagizo hayo kwa kuwaandikia barua watumishi hao. Jana mchana, Waziri Mkuu alifanya ziara ya kushtukiza kwenye bandari ya Dar es Salaam akiwa na nia ya  kukagua namna shug...

Majipu Matano SUGU Anayotakiwa Kuyatumbua Rais Magufuli .....

Image
Wasomi, wanasiasa na watu kutoka makundi mengine ya jamii wamesema Rais John Magufuli atapimwa katika miaka mitano ijayo kwa mambo makubwa matano yaliyoonekana kuwa ‘majipu sugu’ na changamoto kwa mtangulizi wake, Jakaya Kikwete. Majipu (mambo matano) hayo ni ; 1.K udhibiti mtandao wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya . 2. K ukomesha rushwa na ufisadi . 3. K ufumua mtandao wa majangili . 4. K uhakikisha Katiba Mpya inapatikana na  5. K uua ‘mchwa’ unaoitafuna fedha za Serikali. Maoni yaliyotolewa na wasomi, wanasiasa na wananchi wa kawaida yanaonyesha kwamba kufanikiwa kwake kutategemea aina ya ushirikiano atakaoupata kutoka kwa wananchi na wanasiasa na hasa wa kutoka chama chake. Mhadhiri kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Elijah Kondi alisema Dk Magufuli anahitaji kupigana vita kali kufanikisha ahadi zake na akaonya kuwa hawezi kusimama mwenyewe na kushinda vita hiyo bila kuungwa mkono na wananchi hasa chama chake, CCM. “Vigogo ...