Kimbunga kikali chawasili Marekani mashariki
Kimbunga kikali cha
theluji kinachobashiriwa kuwa kikubwa zaidi kwa muda wa miaka mia moja
kimewasili katika ufukwe wa Mashariki mwa Marekani.
Afisi za wafanya kazi wa Serikali na shule zilifungwa mapema na huduma za usafirishaji pia kusitishwa.
Mwandishi wa BBC alisema kuwa mji huo ni kama uliohamwa kwa kuwa watu wote wamejifungia manyumbani hadi kimbunga hicho kitakapopita.
Mji wa New York pia umetangaza hali ya hatari ya hali ya hewa.
Kumekuwa na visa zaidi ya 1,000 vya magari kugongana katika Caroline Kaskazini pekee.
Zaidi ya watu milioni 50 wameonywa kuwa watarajie barafu ya kina cha zaidi ya futi mbili, itakayoongezeka kutokana na kimbunga na upepo mkali utakaovuma saa chache zijazo.
Comments
Post a Comment