Lupita Nyong'o » Oscar » George Clooney, Lupita Nyong’o Waungana na Spike Lee na Jada Pinkett Kulalamikia Tuzo za Oscar Kutawaliwa na Watu Weupe

Washindi wa tuzo za Oscar, George Clooney na Mkenya, Lupita Nyong’o pamoja na muigizaji wa Uingereza David Oyelowo wameungana na mastaa wengine waliopaza sauti kutaka kuwepo mabadiliko kwenye tasnia ya filamu na akademi ya sanaa ya picha zitembeazo na sayansi ambayo wajumbe wake walitaja majina ya waigizaji weupe tu kwenye tuzo za Oscars 2016 kwa mwaka wa pili mfululizo.
Clooney alisema kuwa Academy ilikuwa ikifanya vizuri zaidi miaka 10 iliyopita ambapo waigizaji weusi walikuwa wakipata nafasi.
Muongozaji wa filamu Spike Lee, anayeongoza wito wa kuzisusia tuzo hizo ametaka kuwepo kwa hatua stahiki ili kuleta usawa katika matabaka mbalimbali kwenye Hollywood.
Lee, aliyewahi kupewa tuzo ya heshima ya Oscar, amedai kuwa Hollywood ipo nyuma ya muziki na michezo katika kutambua watu wa matabaka mengine tofauti na weupe.
Mwingine aliyepo mstari wa mbele ni Jada Pinkett-Smith, mke wa Will Smith aliyeigiza filamu ya Concussion ambayo haijatajwa kwenye tuzo hizo. Jada amedai kuwa pamoja na watu weusi kutumika kukabidhi tuzo na kuburidisha, tuzo hizo zimeshindwa kutambua mchango wanaoufanya kwenye filamu zao.
Naye Lupita ametumia Instagram kupost ujumbe huu:
Pinkett na Lee wamesema hawatahudhuria tuzo hizo zitakazotolewa February 28. Asilimia 94 ya wajumbe wa academy hiyo yenye watu zaidi ya 6,000 ni weupe na asilimia 77 ni wanaume.
Hivi karibuni Academy imeanza kuongeza wajumbe wapya wakiwemo host wa tuzo hizi mwaka huu, Chris Rock, Lupita Nyong’o, muongozaji wa filamu ya Selma, Ava DuVernay, mchekeshaji Kevin Hart na Steve McQueen, muongozaji wa filamu ya , 12 Years a Slave.

Comments

Popular posts from this blog

TAZAMA PICHA 30 ZA MREMBO AGNES MASOGANGE AKIJIACHIA KISTAA NJE YA NCHI

Gamboshi: Makao Makuu ya Uchawi na Wachawi yaliyopo Shinyanga, Tanzania

14 parties want Parliament to discuss Zanzibar impasse