Burundi yafanyiwa kikao Addis
Burundi yafanyiwa kikao Addis Ababa
Mabalozi wa Baraza
la Usalama la Umoja wa Mataifa wanafanya mazungumzo kuhusu msukosuko wa
Burundi na viongozi wa Umoja wa Afrika katika mji mkuu wa Ethiopia,
Addis Ababa.
Mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Samantha Power, alisema mazungumzo hayo hayakufanikiwa kama alivyotaraji.
Rais Nkurunziza alikataa wito wa mazungumzo, upatanishi na kikosi cha Umoja wa Afrika kuingilia kati.
Comments
Post a Comment