KAULI za Angelina Mabula baada ya kuteuliwa nafasi ya unaibu waziri na Rais MAGUFULI…

Dec 10 Rais wa awamo ya tano Dr.John Pombe Magufuli aliteuwa rasmi baraza la mawaziri, miongoni waliotajwa ni mbunge wa Ilemela Angelina Mabula ambaye aliteuliwa katika nafasi ya naibu waziri wa Ardhi.
Sasa mbunge huyo amefanya exclusive interview na ripota wa millardayo.com baada ya kuteuliwa katika nafasi hiyo ya kuwa naibu waziri…’Kwanza namshukuru Mungu…pili namshukuru Rais wa awamo ya tano kunichagua katika nafasi ya unaibu kwa wana ilemela niseme tu kwamba nawashukuru tu wao kwasababu wasingenipa nafasi ya ubunge nisingefika hapa nilipo kwahiyo ningependa kuwaambia kwamba tupo bega kwa bega’ – Angelina
‘Naomba nikuhakikishia kwamba mimi sio kati ya wale wanaojisahahu kwasababu  dhamana hii niliyopewa ya unaibu waziri ina mikono ya wana ilemela kwahiyo niseme kwamba nitakuwa pamoja maana unapokuwa waziri au naibu waziri kuna vipindi ambavyo vipo unatakiwa kuwa jimboni…sikutarajia nafasi ya kuwa naibu waziri ila kwasababu Mh Rais kuniaminia ndio maana akanipatia hiyo nafasi’ – Angelina Mabula

Comments

Popular posts from this blog

TAZAMA PICHA 30 ZA MREMBO AGNES MASOGANGE AKIJIACHIA KISTAA NJE YA NCHI

Gamboshi: Makao Makuu ya Uchawi na Wachawi yaliyopo Shinyanga, Tanzania

14 parties want Parliament to discuss Zanzibar impasse