Mgogoro kuhusu kurudiwa kwa uchaguzi viswani Zanzibar unazidi kupasua nchi, sasa viongozi wa Dini ya Kiislam wametofautiana. Sheikh Ponda Issa Ponda Apinga Uchaguzi Kurudiwa Zanzibar
Mgogoro kuhusu kurudiwa kwa uchaguzi viswani Zanzibar unazidi kupasua nchi, sasa viongozi wa Dini ya Kiislam wametofautiana.
Ikiwa
ni siku moja baada ya Alhad Mussa Salum ambaye ni Sheikh Mkuu wa Dar es
Salaam kuunga mkono Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar (ZEC) kutangaza tarehe
ya uchaguzi visiwani humo, Jumuiya ya Taasisi za Kiislam Tanzania imepinga.
Sheikh
Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu nchini
katika mkutano wake na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
amesema, kuruhusu kurudiwa kwa uchaguzi visiwani humo ni kupandikiza
mbegu za chuki kwa wananchi.
Sheikh
Ponda amesema kuwa uchaguzi uliofanyika Oktoba mwaka jana haukuwa na
mashaka kwa kuwa, waangalizi wa nje pia walithibitisha hilo.
“Ripoti za waangalizi wa ndani na nje zilithibitisha kuwa uchaguzi haukuwa na dosari. Kuna sababu gani ya kurudia uchaguzi,” amehoji Sheikh Ponda.
Wakati Sheikh Ponda akihoji sababu za ZEC kutaka kurudiwa kwa uchaguzi huo, Sheikh Alhad aliipongeza tume hiyo na kuongeza “tunaiomba ZEC kusimamia kazi hii kwa haki, uadilifu na umakini mkubwa…”
Sheikh
Alhad jana alisema kuwa Baraza la Waislam Tanzania (BAKWATA) linaunga
mkono uamuzi wa ZEC kurudia uamuzi huku akikitaka Chama cha Wananchi
(CUF) ambacho kimesusia uchaguzi huo, kushiriki.
CUF
kwenye mkutano wake wa Baraza Kuu uliofanyika tarehe 27 na 28 Januari
mwaka huu kilieleza kususia uchaguzi huo uliopangwa kufanyika tarehe 20
Machi mwaka huu na kudai kuwa, hakuna sababu yoyote kwa chama hicho
kushiriki. ZEC ilifuta uchaguzi huo tarehe 28 Oktoba mwaka jana.
Hata
hivyo, Sheikh Ponda amesema kuwa, ZEC haikuwa na sababu ya kufuta
uchaguzi kwa kuwa, baada ya tume hiyo kutangaza matokeo, haina mamlaka
ya kufuta.
Pamoja na kupinga kurudiwa kwa uchaguzi, Sheikh Ponda Sheikh Alhad amepata wapi kauli ya
Kiongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar
(Jumiki), Sheikh Farid Hadi Ahmed kuwa anaunga mkutano marudio ya
uchaguzi Zanzibar.
Sheikh Alhad kwenye mkutano wake jana alisema “Hata
kiongozi wa Uamsho, Sheikh Farid Ahmad pia anaunga mkono suala la
kufanyika uchaguzi wa marudio kwa mujibu wa barua yake aliyonitumia mimi
.”
Sheikh
Ponda ameeleza kwamba, Sheikh Farid hawezi kutoa kauli hiyo na kwamba
kama Sheikh Alhad anayo barua hiyo, aitoe hadharani.
“Sio
jambo rahisi kuamini kwamba Sheikh Farid anaweza kutoa kauli hiyo, sio
jambo rahisi kabisa na kama ni kweli basi atoe ushahidi wake,” ameeleza Sheikh Ponda.
Pia
Sheikh Ponda ameonesha kushangazwa na ZEC kuhalalisha matokeo ya Rais
wa Muungano wa Tanzania sambamba na Wabunge wa Bunge la Muungano.
Shekh Ponda amesema kuwa uchaguzi wa Zanzibar na matokeo yake bado ni halali “Sisi kama Tasisi ya Waislamu tunapinga kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar.”
Amesema
kuwa, taasisi hiyo imeunga mkono hatua za mwanzo zilizochukuliwa na CUF
pia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kunusuru hali ya kisiasa visiwani humo na
kutaka majadiliano yaendelee.
Shekh
Ponda amemshauri Rais John Magufuli kutimiza ahadi yake aliyoitoa
bungeni ya kushughulikia mzozo huo kwa kushirikiana na Maalim Seif
Shariff Hamad na Dk. Ali Mohammed Shein.
Amesema kuwa, Rais Magufuli hajatoa tamko lolote na kwamba hajaeleza amefikia wapi katika kutatua mzozo huu.
Sheikh
Ponda amesema kuwa kuna viashiria vya kuvunjika kwa amani visiwani humo
kutokana na watu kuporwa haki zao na kwamba watakapoamua kuitafuata
kutazuka vurugu.
Comments
Post a Comment