Chadema yalaani vurugu chaguzi za meya, wenyeviti halmshauri.
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), George Simbachawene.
Pia kimemtaka aliyesimamia uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri
Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro, Yahya Nania, kuonyesha barua
iliyotoka kwa Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), George Simbachawene, inayosema kuwa Peter Lijualikali
haruhusiwi kupiga kura katika halmashauri hiyo wakati ni Mbunge wa Jimbo
la Kilombero.
Chadema kimeonya asipofanya hivyo kitamshitaki mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuhatarisha amani jimboni humo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Naibu
Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu, alisema msimamizi huyo
wa uchaguzi kumtaka Lijualikali kuchagua sehemu ipi ya kupiga kura ni
kukiuka sheria na kanuni za Tamisemi, kwani sheria inamruhusu mjumbe wa
sehemu husika kushiriki uchaguzi.
“Mgawanyo wa mipaka ya Jimbo la Kilombero ni kama Jimbo la Kyela
ambalo ndani ya jimbo hilo kuna Mamlaka ya Mji Mdogo Kyela na
Halmashauri ya Wilaya ya Kyela na Mbunge wa jimbo hilo alikuwa
akishiriki chaguzi zote za kumpata mwenyeki bila pingamizi kama ilivyo
sasa," alisema Mwalimu.
Wakati huo huo Chadema kimemshauri Meya wa Manispaa ya Kinondoni,
Boniface Jacob, kuandika barua kwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
kuomba ufafanuzi kuhusu uhalali wa majina ya wajumbe wapya 11 kutoka nje
ya Dar es Salaam kuruhusiwa kushiriki uchaguzi wa kumpata Meya wa jiji
hilo.
Mwalimu alisema endapo tume hiyo itajibu kwamba wajumbe hao ni
halali chama kitajua cha kufanya na endapo itathibitika kwamba barua
kuhusu suala hilo haikutoka tume, hatua kali za kisheria zitachukua
mkondo wake kwa waliohusika.
Comments
Post a Comment