WhatsApp Skype Zaleta Mvutano Afrika Kusini>>> Soma Zaidi HAPA>>

Mvutano kuhusu WhatsApp Afrika Kusini                                                                                        
 
 
Kampuni kubwa za kutoa huduma za mawasiliano nchini Afrika Kusini zimeitaka tume inayoisimamia mawasiliano ya nchi hiyo kudhibiti matumizi ya programu za mawasiliano ya mitandao ya kijamii kama vile WhatsApp na Skype.

Maafisa wakuu wa kampuni ya MTN na Vodacom walifika mbele ya kamati ya bunge la Afrika Kusini wakitaka huduma ya bei nafuu ya intaneti inayotambuliwa kama over-the-top (OTT) internet , idhibitiwe.

Kauli yao hata hivyo ilipingwa na kampuni ya Cell C inayodai kuwa makampuni hayo makubwa yanalenga kukandamiza mawasiliano na ubunifu.

MTN na Vodacom zinatoa hoja kuwa huduma ya mitandao hiyo ya OTT zinatumia mitandao yao pasi na malipo kamili kwani kwa sasa mtu anaweza kutumia programu hizo WhatsApp na Skype kupiga simu.

Kamati hiyo ya bunge inayosimamia mawasiliano na huduma za posta inatafuta ukweli kuhusu mbinu za kuweka sheria za kuthibiti vyombo vya mawasiliano na huduma za OTT.

Comments

Popular posts from this blog

TAZAMA PICHA 30 ZA MREMBO AGNES MASOGANGE AKIJIACHIA KISTAA NJE YA NCHI

Nimerekodiwa Video ya Ngono Bila Kujijua. Nifanyeje?

Zitto Kabwe » Zitto Kabwe Ayafungukia Makampuni Makubwa Tanzania Ambayo Yanakwepa Kodi....