Umesikia Hii>>>Mbowe ahoji askari wa Bara kupiga kura Z'bar. Soma Zaidi Hpa>>>>ki
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,
Freeman Mbowe.
Akiuliza swali la nyongeza bungeni jana, Mbowe ambaye ni Mbunge wa
Hai (Chadema), alisema kumekuwapo na utamaduni wa kuwatumia askari
kutoka Tanzania Bara na kuwapeleka Zanzibar na kuwaandikisha wakati wa
uchaguzi ili kuwatumia kupiga kura katika mazingira ambayo hayapo wazi.
“Je, waziri una taarifa ya upelekaji wa vikosi Zanzibar kwa jukumu
moja la kupiga kura na baada ya hapo wanarudishwa bara?,” alihoji Mbowe.
Akijibu swali hilo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk.
Hussen Mwinyi, alisema jambo hilo haliwezekani kwani utaratibu wa
kupiga kura upo wazi na unaeleweka.
”Huwezi kwenda leo Zanzibar na kuandikishwa kupiga kura, lazima uwe
ni Mzanzibari mkazi, hilo lipo na ushahidi tunao wanajeshi
wanaopelekwa Zanzibar ni kwa ajili ya kulinda usalama tu nyakati za
uchaguzi si zaidi ya hapo,” alisema Dk. Mwinyi.
Alisema majeshi yaliyopo ni ya Muungano na kwa maana hiyo askari wa
Jeshi la Wananchi wa Tanzania anaweza kupangiwa kufanyakazi sehemu
yoyote ya Jamhuri ya Muungano.
Awali, akijibu swali la msingi la Mbunge wa Jimbo la Shaurimoyo
(CCM), Mattar Salum, aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa utoaji
ajira kwa vijana waliopata mafunzo ya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Dk.
Mwinyi alisema Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania lina utaratibu
wa kuandikisha askari wapya kupitia makambi ya Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU).
Alisema jeshi hilo hutoa nafasi za ajira katika mikoa yote ya
Tanzania Bara na Visiwani, ambako vijana husajiliwa kwa utaratibu
uliowekwa na wale wanaofaulu hupelekwa katika makambi ya jeshi hilo.
Katika swali jingine la nyongeza, Mbunge wa Malindi (CUF), Ally
Sale, alimtaka waziri huyo kueleza kama ana taarifa ya kuwapo kwa rushwa
kubwa zinazotolewa katika kutoa ajira kwenye nafasi za vikosi vya
ulinzi.
Dk. Mwinyi alisema hana taarifa juu ya suala hilo na kumtaka Mbunge
huyo kumpatia majina ya wanaohusika na upokeaji wa rushwa ili hatua
ziweze kuchukuliwa.
Comments
Post a Comment