Wabunge wameitaka serikali kuhakikisha kuwa inaweka msisitizo katika suala la utawala bora.
Wabunge
wameitaka serikali kuhakikisha kuwa inaweka msisitizo katikasuala la
utawala bora kama inania ya dhati ya kulifikisha taifa katika mpango
wake iliyojiwekea sambamba na kuhakisha kuwa, uwekezaji unazingatia
taratibu na sheria zilizopo.
Wakichangia katika mjadala huo ambao unaingia siku ya tatu Mh Saidi
Kubenea mbunge wa Ubungo alisema katika bunge la kumi moja ya mambo
makubwa yaliyoamu liwa ni sakata la fedha za Escrow lakini yapo maamuzi
ambayo hadi sasa hayajafanyiwa kazi na hivyo dhana ya utawla bora
inakuwa haipo.
Aidha Mh Mbaraka dau mbunge wa Mafia amesema kuna visiwa vya
Shungilimbili ambavyo wameuziwa wawekezaji kinyume na taratibu huku mh
Jerome Bwanausi mbunge wa Lulindi akitaka watendaji kuwa wabunifu wa
vyanzo vya mapato.
Awali katika mjadla huo Mh John Heche mbunge wa Tarime vijijini
alisema kitendo cha polisi wa kutuliza ghasia kuingia ndani ya ukumbi wa
bunge kuwadhibiti hakikuwa sahihi.
Kauli hiyo ilipingwa na Mh Livingstone Lusinde mbunge wa Mtera
ambaye alisema kitendo cha polisi kuingia ndani ilikuwa sawa kwani
polisi wanaweza kuingia sehemu yoyote kwa lengo la kuimarisha usalama.
Comments
Post a Comment