Beaking>>+ News >>Nigeria: Milipuko yaua watu Chibok
Watu 13 wameuawa
nchini Nigeria baada ya wapiganaji watatu wa kujitolea muhanga kujilipua
katika mji wa kaskazini mashariki wa Chibok ambapo kundi la Boko Haram
liliwateka nyara zaidi ya wasichana 200 wa shule, kulingana na mzee
mmoja aliyezungumza na chombo cha habari cha AFP.
Mabomu hayo yanadaiwa kulenga maeneo matatu tofauti.
Bomu la kwanza lililipuka katika soko la kila wiki huku jingine likilipuka katika kituo cha barabarani.
Haijajulikana bomu la tatu lililipuka wapi.
Mkaazi mmoja wa Chibok ameiambia BBC kwamba walipuaji watano wa kujitolea muhanga waliingia katika mji huo mapema siku ya jumatano huku watatu kati yao wakijilipua.
Wawili waliosalia bado wako katika mji huo kulingana na Malam Ayouba.
''Watu niliozungumza nao bado wameshangaa'', wengine wao bado wanalia,aliambia idhaa ya BBC Hausa.
Wapiganani kundi la Boko Haram walivamia mji huo mnamo mwezi Aprili 2015 na kuwateka nyara zaidi ya wasichana 200.
Utekaji huo ulizua hisia kali kimataifa.
Comments
Post a Comment