Katibu Mkuu wa Zamani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa ametoa majibu kuhusu taarifa zinazoandikwa>>> Soma Zaidi Hapa
Katibu
Mkuu wa Zamani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.
Wilbroad Slaa ametoa majibu kuhusu taarifa zinazoandikwa kwenye baadhi
ya magazeti nchini pamoja na mitandao kuwa nyumba yake iliyoko Mbezi
jijini Dar es Salaam inauzwa baada ya kushindwa kulipa mkopo wa Benki ikidaiwa kuwa mkewe aliuchukua na kumpa mwanaume mwingine.
Taarifa
hizo zilieleza kuwa Mke wa Dk. Slaa, Josephine alichukua mkopo wa
shilingi milioni 300 katika moja kati mabenki nchini na kushindwa
kuirudisha fedha hiyo.
Dk.
Slaa ambaye yuko nchini Canada akijiendeleza kimasomo, amekanusha
taarifa hizo na kueleleza kuwa yeye na mkewe Josephine hawajawahi
kuchukua mkopo katika benki yoyote nchini.
“Nataka
nikuambie na uwajulishe Watanzania kwamba wala si mimi Dk. Slaa wala
mke wangu, Josephine kwa wakati wowote ule hatujawahi kuchukua mkopo
benki,” Dk. Slaa aliliambia gazeti la Mtanzania kwa njia ya simu.
“Tangu nitoke Bungeni sijawahi kuchukua hata senti moja benki, achilia mbali propaganda ya shilingi milioni 300.
"
Hivyo, ni vizuri waliokupa taarifa wakupe undani ni benki ipi nilikopa
au Josephine alikopa na ni shilingi ngapi na kwa nyaraka zipi.
"Na ni vema ukafuatilia benki husika pia kama walikuwambia ni benki gani,” Mwanasiasa huyo mkongwe alieleza.
Dk.
Slaa ambaye alitangaza mwaka jana kustaafu siasa, alisema kuwa anapanga
kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wote walioandika habari hizo.
Comments
Post a Comment