Wabunge wameitaka serikali kuhakikisha kuwa inaweka msisitizo katika suala la utawala bora.
Wabunge wameitaka serikali kuhakikisha kuwa inaweka msisitizo katikasuala la utawala bora kama inania ya dhati ya kulifikisha taifa katika mpango wake iliyojiwekea sambamba na kuhakisha kuwa, uwekezaji unazingatia taratibu na sheria zilizopo. Wakichangia katika mjadala huo ambao unaingia siku ya tatu Mh Saidi Kubenea mbunge wa Ubungo alisema katika bunge la kumi moja ya mambo makubwa yaliyoamu liwa ni sakata la fedha za Escrow lakini yapo maamuzi ambayo hadi sasa hayajafanyiwa kazi na hivyo dhana ya utawla bora inakuwa haipo. Aidha Mh Mbaraka dau mbunge wa Mafia amesema kuna visiwa vya Shungilimbili ambavyo wameuziwa wawekezaji kinyume na taratibu huku mh Jerome Bwanausi mbunge wa Lulindi akitaka watendaji kuwa wabunifu wa vyanzo vya mapato. Awali katika mjadla huo Mh John Heche mbunge wa Tarime vijijini alisema kitendo cha polisi wa kutuliza ghasia kuingia ndani ya ukumbi wa bunge kuwadhibiti hakikuwa sahihi. Kaul...