Posts

Showing posts from November, 2015

» Mapenzi » Media Bar » Slider » Madhara ya Kutofanya Tendo la Ndoa Muda Mrefu.

Image
Madhara ya Kutofanya Tendo la Ndoa Muda Mrefu. Habari zenu, nimeona niwaletee hili nina imani mtajifunza hasa kwa wale wasiofahamu,Ukikaa Muda Mrefu bila Kufanya tendo la Ndoa madhara yake ni kama haya: • Hasira za mara kwa mara katika mambo madogo, • kupendelea sana kuangalia picha za uchi, • Kusahausahau, • Kupendelea story za mapenzi, • Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi (Mke), • Kupenda kurukiarukia mambo ya watu wengine (tabia ya kufuatilia mambo yasiyokuhusu), • Kuumwa na kichwa, • Kukakamaa mgongo (wanaume), • Kuingiliwa kirahisi na jini mahaba, • Kupoteza umakini ktk kazi (efficiency), • Siku ukikutana kimwili na mwenye virusi bila kinga utaambukizwa kirahisi mno, • Waweza ku-develop tabia mpya ambayo hukuwahi kuwa nayo ili iwe mbadala kama ulevi n.k.

» CCM » CCM Yakanusha Taarifa za Kuridhia Kuapishwa kwa Maalim Seif Kuwa Rais wa Zanzibar

Image
CCM Yakanusha Taarifa za Kuridhia Kuapishwa kwa Maalim Seif Kuwa Rais wa Zanzibar Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekanusha taarifa iliyosambazwa kupitia mitandao ya kijamii ya kuridhia Mgombea wa Chama Cha (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad atangazwe kuwa Rais wa Zanzibar. Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Kisiwandui mjini hapa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema wamepokea kwa msikitiko makubwa taarifa hizo alizoziita za uzushi. Alisema chama chake hakipo tayari kuvunja katiba wala sheria kwa kuridhia kuwa Maalim Seif atangazwe, kwani uchaguzi uliofanyika tayari umefutwa rasmi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kupitia Gazeti la Serikali. " Mtandao huo wa kijamii ulidai kuwa mimi Naibu Katibu Mkuu niliwataka wananchama na wananchi wote kuridhia hatua hiyo iliyofikiwa ya chama chetu kuridhia kuapishwa Maalim Seif , huku nikisisitiza kwa kuwataka wananchi wote wajitokeze kwa wingi katika sherehe za...

John Magufuli » Kimbunga cha Magufuli chatua Mashirika ya Umma, ATCL, TRL And Tazara Matumbo Moto

Image
Kimbunga cha Magufuli chatua Mashirika ya Umma, ATCL, TRL And Tazara Matumbo Moto Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru amezitaka taasisi na mashirika ya umma nchini kuacha utegemezi kwa Serikali, badala yake kupunguza matumizi na wafanyakazi ili kuongeza mapato na ufanisi. Mafuru alisema Serikali imebeba mzigo wa taasisi na mashirika hayo kwa kutegemea izipatia fedha kutoka Hazina kwa ajili ya kujiendesha, na kulipa mishahara ya wafanyakazi na kusababisha ufanisi wao kuwa mdogo. Mafuru pia alitangaza kufuta posho za wabunge katika bodi za mashirika na kuanzisha mchakato wa kuwaondoa katika mashirika hayo, ili wabaki na jukumu lao la msingi la kuikosoa Serikali badala ya kuingia katika utendaji. Kuhusu uzalishaji Msajili huyo alisema inashangaza kuona kwamba mpaka sasa kuna mashirika ya umma ambayo bado yanaitegemea Serikali kulipa mishahara ya wafanyakazi wake. Aliyataja mashirika hayo kuwa ni Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Kampuni ya Hifadhi ...

Kenyan News » Kenyan Guy Narrates The Trick a Desperate Single Mother Used to Seduce Him To S£X (PICTURED)

Image
Kenyan Guy Narrates The Trick a Desperate Single Mother Used to Seduce Him To S£X (PICTURED) A Kenyan guy has narrated how he visited a desperate single mother, who happens to be his side-dish, and the trick she used to lure him to s3x. This is what he had to say;

Habari za Magazeti » Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Tarehe 1 Disemba...Ikiwemo ya Miss Tanzania Atajwa Ufisadi wa Sh 1.3 Trilioni

Image
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Tarehe 1 Disemba...Ikiwemo ya Miss Tanzania Atajwa Ufisadi wa Sh 1.3 Trilioni

Jaji Utamwa, Fungamtama Uso kwa Uso na David Kafulila Katika Kesi ya Ubunge

Image
KESI ya matokeo ya ubunge katika Jimbo la Kigoma Kusini iliyofunguliwa na David Kafulila, inamkutanisha uso kwa uso na Jaji John Utamwa lakini pia wakili Kennedy Fungamtama.. Fungamtama alikuwa wakili wa Kampuni ya Dowans katika kesi dhidi ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco) wakati Jaji Utamwa ndiye aliyetoa hukumu ‘tata’ ya kesi ya kampuni ya kufua umeme wa dharura (IPTL) mwaka 2013 iliyozaa sakata la ufisadi kwenye Akaunti Escrow. Kwenye kesi ya Dowans dhidi ya serikali (Tanesco), Wakili Fungamtama akiitetea Dowans alishinda wakati katika kesi ya IPTL, Jaji Utamwa alitoa hukumu inayotajwa kuwa chanzo cha sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh. 306 bilioni kwenye Akaunti ya Esrcow bungeni mwaka 2014. Hatua ya kuchotwa kwa fedha hizo ndiyo iliyomuibua Kafulila ambapo alidai kuwepo kwa ufisadi katika uchotaji huo. Katika kesi ya uchaguzi ya Kafulila, wakili Fungamtama amesimama kumtetea mbunge wa jimbo hilo, Hasna Mwilima aliyetangazwa kushindwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (C...

Magufuli Azipiga Chini Posho za Wabunge......Posho za Mikutano ya Bodi Ya Mashirika Ya Umma Nazo Zimepigwa Chini

Image
Mpango wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dk. John Magufuli, kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ili fedha zitumike kuboresha huduma za jamii, umetua kwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao sasa wameondolewa malipo ya posho wakati wanapokuwa katika vikao vya kamati zao mbalimbali za kisekta. Kwa muda mrefu sasa, imezoeleka kwa wabunge kupokea posho kutoka kwenye mashirika na taasisi mbalimbali za umma wanapoketi kutekeleza wajibu wao ndani ya kamati za Bunge.  Hata hivyo, posho hizo hazitakuwapo tena baada ya Msajili wa Hazina, Lawrance Mafuru, kutangaza jana kuwa sasa posho hizo hazitatolewa tena kwani wanachokifanya wabunge ni sehemu ya kazi zao. Msajili alitoa agizo hilo wakati wa mkutano wake na wakuu wa taasisi na mashirika ya umma na pia wenyeviti wa bodi zao. Msajili Mafuru alisema agizo hilo limetoka kwa Rais Magufuli, na kwamba sasa kinachotakiwa ni kuona utekelezaji wake. Bodi zafutiwa Posho za Vikao Kadhalika, Mafuru alisema serikali imefut...

Kashfa Nzito ya Ufisadi Wa Trioni 1.2/- Katika Serikali ya JK Yaibuliwa na Zitto Kabwe

Image
Serikali ya Uingereza kupitia shirika lake la kuchunguza makosa ya jinai (AFO), imeibua kashfa ya rushwa katika ununuzi wa dhamana (hati fungani) ya serikali katika kipindi cha uongozi wa aliyekuwa Rais Jakaya Kikwete. Madai hayo yametolewa jijini Dar es Salaam jana na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, katika taarifa yake aliyoisambaza kwenye vyombo vya habari jana. Katika taarifa yake hiyo, Zitto alidai kuwa biashara hiyo iliyofanyika kati mwaka 2011 na 2012, iliyohusisha serikali na benki ya Standard Group ya Afrika Kusini kupitia Stanbic ya Tanzania ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani milioni 600 (sawa Sh. Tanzania trioni 1.2). Benki ya Standard Group ambayo ni benki mama ya Stanbic Tanzania, imekiri makosa hayo na kukubali kulipa faini ya Dola milioni 25.2 (sawa na Sh. bilioni 54 ) kwa kosa hilo. Ilikubali kulipa faini hiyo mbele ya Jaji Lord Justice Leveson, wakati shauri hilo liliposikilizwa jana kwenye Mahakama ya Southwark nchini Uingereza...

Ripoti kutoka mahakamani Nigeria kuhusu kesi ya Mchungaji T B Joshua…

Image
Mchungaji wa Kanisa la Church of All Nations Nigeria , TB Joshua na Wakandarasi wawili ambao wanakabiliwa na mashtaka ya uzembe uliopelekea jengo la Kanisa hilo kuanguka na kusababisha vifo vya watu 116, leo wameshindwa kufika Mahakamani kusikiliza kesi inayowakabili kuhusu vifo vya watu hao. Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakama Kuu ya Lagos Nigeria baada ya tukio la kuanguka kwa jengo la kufikia wageni lililopo kwenye Kanisa la TB Joshua September 12 2014 na kupelekea vifo hivyo ambapo kati ya waliofariki, 81 walikuwa raia wa Afrika Kusini. Katika Mashtaka yaliyofunguliwa Mahakamani, Kanisa hilo limedaiwa kufanya ujenzi wa jengo hilo la ghorofa sita bila kuwa na kibali cha kufanya ujenzi huo. Kwa upande wa TB Joshua wamekuwa wakijitetea kwamba sababu ya jengo hilo kuanguka inatokana na ndege moja ambayo ilizunguka juu ya jengo hilo, muda mfupi baadae jengo hilo likaanguka.. anaamini kuna hujuma zilizofanywa kwenye tukio hil...

General News Baada ya moto wa Magufuli kupita bandarini, hii ndio idadi ya waliokamatwa mpaka sasa..

Image
Ijumaa November 27 2015 Waziri Mkuu mpya wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa alifanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam na kuwasimamisha kazi maofisa watano wakihusishwa na ubadhirifu na kutowajibika. Muda mfupi baadae siku hiyohiyo, aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato TRA pia alisimamishwa kazi, lilikuwa ni agizo la Waziri Mkuu huyo kwamba yeyote aliyehusishwa na ubadhirifu akamatwe na uchunguzi uendelee juu yake. Nimeipokea Ripoti nyingine kutoka Jeshi la Polisi ambapo watu 12 wanashikiliwa mpaka sasa wakihusishwa na tuhuma za ubadhirifu bandarini Dar es Salaam. Wahusika hao hawajatajwa majina kwa sababu ya upelelezi unaoendelea, ninayo hapa ripoti ya kituo cha TV ya Channel Ten kuhusu taarifa ya kukamatwa maofisa hao.

Zitto Kabwe » Zitto Kabwe Ayafungukia Makampuni Makubwa Tanzania Ambayo Yanakwepa Kodi....

Image
Zitto Kabwe Ayafungukia Makampuni Makubwa Tanzania Ambayo Yanakwepa Kodi.... By Zitto Kabwe Kutoka Hotuba ya Waziri Mkuu 26.08.2011 – Makampuni yanayoogoza kwa kulipa kodi Note: (Highlights) Only one Mining company (the smallest i.e. - Resolute Mining), only one telecom company(Airtel Tanzania). Household names like:  MeTL, Bakhresa/Azam, IPP, VodaCom, Coca cola, Pepsi(SABCO), Serengeti Breweries, Barrick Gold, ACACIA, AngloGold Ashanti not seen. No oil marketing companies pia. One can conclude that, TBL is the most profitable company in Tanzania, NMB is the most profitable Bank. A public debate is needed. Hili ni tatizo kubwa. Here under is the an extract from the Prime Minister speech; Sehemu ndogo ya hotuba ya Waziri mkuu. Mheshimiwa Spika, 1. Nitumie nafasi hii kuwapongeza baadhi ya Walipakodi Wakubwa kwa Serikali na ambao wamefanya vizuri kati ya kipindi cha mwaka 2005 na 2011. Kwa kipindi hicho, Makampuni yaliyoongoza kwa kulipa kodi ni pamoja na: Tanzania Breweries Ltd....

Ajira » Nafasi za Kazi Tanzania Posts Corporation, Assistant Postal Officers (8 Posts) And Senior Economist II

Image
Nafasi za Kazi Tanzania Posts Corporation, Assistant Postal Officers (8 Posts) And Senior Economist II Ingia Kwenye Website Ifuatayo Uweze Ku Apply Kazi Hizo zilizotangazwa Katika Gazeti la leo la Daily News =>>   www.ajirayako.com

Rais Magufuli Akutana na Mabolozi Wa China na Korea Kusini........Ahakikishiwa Ujenzi wa Daraja la Salender Dar

Image
Vichwa vya habari za siasa Tanzania bado vinaendelea kubeba stori kila mara kuhusu Rais Magufuli … inawezekana ni kawaida kabisa kila siku kukutana na habari zaidi ya tatu au nne kuhusu Rais Magufuli tangu siku ya kwanza alipoapishwa na kuanza kazi ya Urais wa Tanzania.   Ninayo nyingine kutoka Ikulu sasahivi, hii inahusu Rais Magufuli kumuaga Balozi wa Korea Kusini, Chung IL ambapo Balozi huyo amemhakikishia Rais Magufuli kwamba daraja hilo litajengwa kwa ufadhili wa Serikali yake. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Korea ya Kusini hapa nchini Mhe. Chung IL, Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015. Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing, Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015. Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo  na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing, Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015.

» Rais Magufuli kaamua Bilioni zilizokua zitumike sherehe za uhuru 9 Dec matumizi yake yawe kama ifuatavyo.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru fedha zilizopaswa kutumika kugharamia shamra shamra za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika tarehe 09 Desemba 2015, kutumika kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami. Tayari fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni nne zimepelekwa kwa wakala wa barabara hapa nchini TANROADS kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo, linalopaswa kuanza mara moja Akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi PATRICK MFUGALE Ikulu Jijini Dar es Salaam, Dkt. Magufuli ametaka ujenzi wa barabara hiyo uanze haraka ili kukabiliana na adha ya msongamano wa magari katika barabara hiyo Kujengwa kwa njia hizo kutaifanya barabara ya Morroco hadi Mwenge kuwa na njia tano. Wakati huo huo, Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba Ikulu Jijini Dar es salaam. ...

Samia Hassan Suluhu » Rais John Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa Wamuibukia Samia Suluhu Hassan Ofisini Kwake

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akiagana na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015. Wa pili (kulia) ni Naibu Katibu wa Makamu wa Rais, Mohamed Khamis Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, (kushoto) akizungumza na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, wakati Rais na Waziri Mkuu walipomtembelea Makamu Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015 kwa mazungumzo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, (kushoto) akizungumza na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, wakati Rais na Waziri Mkuu walipomtembelea Makamu Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015 kwa mazungumzo.

Upotevu wa Makontena 349 Bandarini: Watu 12 Watiwa Mbaroni na Jeshi la Polisi

Image
Kufuatia agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kuwataka watuhumiwa wa wizi wa makontena 329 katika bandari ya Dar es salaam kuchukuliwa hatua na Jeshi la Polisi, tayari Jeshi hilo limewashikilia watuhumiwa kumi na mbili wanaohusika na wizi huo. Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam,  Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CP) Diwani Athumani amesema kuwa, uchunguzi unaofanywa na wataalamu waliobobea katika makosa ya uhalifu wa kifedha umeweza kuwabaini watu kumi na mbili  ambao wamehusika na wizi huo. “Kati ya watuhumiwa hao kumi na mbili, watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na saba bado wapo katika upepelezi na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani,” alisema Kamanda Athumani. Wanaoshikiliwa kutokana na tuhuma mbalimbali ni Kamishna wa Idara ya Forodha na Ushuru TRA Bw. Tiagi Masamaki, Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru  na Bi.  Habib Mponezia, Msimamizi Mkuu wa Kitengo cha Ushuru wa Forodha. Watuhumiwa ...

UNA YAJUA Magoli matatu yaliofanikiwa kuingia fainali ya goli bora la mwaka 2015 la FIFA? na Messi yupo (+Video)

Image
Baada ya November 7 shirikisho la soka ulimwenguni FIFA kutangaza magoli 10 yaliofanikiwa kuingia katika mchujo wa kuchagua goli bora la mwaka 2015, November 30 ndio siku ambayo yachujwa na kubakia magoli matatu pekee ambayo January 11 2016  Zurich Uswiss   wakati wa utoaji wa Tuzo ya Ballon d’Or ndio litatangazwa goli bora kwa mwaka 2015. Lionel Messi Wachezaji watatu ambao magoli yao yamefanikiwa kuingia katika hatua hiyo ni  Alessandro Florenzi kutokea AS Roma , Lionel Messi wa FC Barcelona na Wendell Lira wa klabu ya  Vila Nova . Alessandro Florenzi Wendell Lira Video ya goli la W endell Lira Video ya goli la  Alessandro Florenzi Video ya Lionel Messi

Exclusive Interview: Kassim Mganga on air with Millard Ayo (video)

Image
Kassim Mganga ni miongoni mwa wakali wenye majina yao ndani ya bongofleva, akiwa na hits kama ‘ awena ‘ ‘ I love you ‘ na nyingine, alipata time na akapita TZA kwenye studio za Millard Ayo na kufanya Interview ya mengine mengi ambayo hatujawahi kumsikia akiyaongea.

Baada ya majina 23 kuchujwa, hawa ndio mastaa watatu waliofanikiwa kuwania tuzo ya Ballon d’Or!!

Image
Mastaa watatu wa soka duniani Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Neymar wamerudi kwenye headlines baada ya kuchaguliwa kushindania tuzo ya kimataifa ya mwaka ya Ballon d’Or. Huu unakuwa mwaka wa nane kwa staa wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo na Lionel Mess kushiriki katika tuzo hizo kubwa duniani. Mshindi wa tuzo hizo anatarajiwa kutangazwa rasmo katika jiji la Zurich, Uswis January 11 2016. Mastaa hao watatu wamefanikiwa kutangazwa  baada ya kushindanishwa kati ya wachezaji 23 waliokuwa wakiwania akiemo Wales na Gareth Bale. Pia makocha watatu watakaowania tuzo hiyo na timu zao kwenye mabano ni Pep Guardiola (Spain/FC Bayern Munich), Luis Enrique Martínez (Spain/FC Barcelona), Jorge Sampaoli wa (Argentina/Chilean national team) Hawa ndio mastaa waliokuwa wakiwania tuzo hiyo. 1. Sergio Aguero (Argentina/Manchester City) 2.Gareth Bale (Wales/Real Madrid) 3.Karim Benzema (France/Real Madrid) 4.Cristiano Ro...

Rais Magufuli alivyohakikishiwa ujenzi wa daraja la Salender Dar..

Image
Vichwa vya habari za siasa Tanzania bado vinaendelea kubeba stori kila mara kuhusu Rais Magufuli … inawezekana ni kawaida kabisa kila siku kukutana na habari zaidi ya tatu au nne kuhusu Rais Magufuli tangu siku ya kwanza alipoapishwa na kuanza kazi ya Urais wa Tanzania. Rais Magufuli akionesha ramani ya daraja la Salender , enzi hizo alikuwa Waziri wa Ujenzi . Ninayo nyingine kutoka Ikulu sasahivi, hii inahusu Rais Magufuli kumuaga Balozi wa Korea Kusini, Chung IL ambapo Balozi huyo amemhakikishia Rais Magufuli kwamba daraja hilo litajengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Korea Kusini. Daraja hilo litajengwa kuunganisha eneo la Coco Beach na Ocean Road ambapo litakuwa na urefu wa kilometa 6.3.

Kipigo cha Ethiopia cha warejesha Kilimanjaro Stars Tanzania, Full Time ya CECAFA Nov 30 …

Image
Michuano ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati maarufu kama CECAFA Senior Challenge Cup yameendelea leo November 30 kwa kupigwa mechi za kwanza za robo fainali ya michuano hiyo, miongoni mwa mechi za robo fainali zilizochezwa leo November 30 ni mechi kati ya timu ya taifa ya Tanzania bara maarufu kama Kilimanjaro Stars ilicheza dhidi ya mwenyeji wa mashindano hayo timu ya taifa ya Ethiopia . Hii ni mechi ya robo fainali iliyokuwa inazikutanisha timu zilizokuwa kundi moja na mchezo wao wa mwisho walicheza na kumaliza kwa sare ya goli 1-1, November 30 Kilimanjaro Stars ilicheza mchezo huo ikiwa na kikosi chake kamili lakini kilikuwa na mabadiliko kidogo. Mchezo huo ambao Kilimanjaro Stars walianza kwa kupata goli la kuongoza kupitia kwa nahodha wao John Bocco dakika ya 24, dakika 90 zilimalizika kwa sare ya goli 1-1 baada ya Panom Cathuoch  kuisawazishia goli Ethiopia dakika 57 . Kwa kawaida ya michuano hiyo kw...