KIJIJI CHA GAMBOSHI 'MAKAO MAKUU YA UCHAWI NA WACHAWI' NI MKOA WA SHINYANGA. USIKU YAONEKANA KAMA JIJI LA NEW YORK AU LONDON.WENYEWE WAMWOMBA RAIS KIKWETE, MZEE WA VIJISENTI AKAWASAFISHE. Gari linalokokotwa na ng'ombe katika barabara ya kuelekea kijijini Gamboshi. WAKAZI wa Kijiji cha Gamboshi, kilichopo wilayani Bariadi, Mkoa wa Shinyanga, wamemuomba Rais Jakaya Kikwete awasaidie kusafisha kijiji chao kutokana na jina baya lililoenezwa duniani kwamba hapo ni makao makuu ya maovu ya uchawi ulioshindikana. Kijiji hicho ambacho ni nadra sana kutembelewa, kimepata umaaurufu mkubwa ndani na nje ya nchi kikielezwa kuwa ni kitovu cha uchawi na wachawi wanaoweza kufanya miujuza, hali ambayo imekifanya kijiji hicho kupitwa na mkondo wa kimaendeleo. “Sisi ni wakulima wakarimu wa pamba, mahindi na mpunga. Yote mnayoyasikia kwamba sisi ni magwiji wa uchawi ni uvumi uliotiwa chumvi nyingi.Tunamwomba Rais wetu kwakushirikiana na Mbunge wetu,And...
Comments
Post a Comment