General News Baada ya moto wa Magufuli kupita bandarini, hii ndio idadi ya waliokamatwa mpaka sasa..
Ijumaa November 27 2015 Waziri Mkuu mpya wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa alifanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam na kuwasimamisha kazi maofisa watano wakihusishwa na ubadhirifu na kutowajibika.
Muda mfupi baadae siku hiyohiyo, aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato TRA pia alisimamishwa kazi, lilikuwa ni agizo la Waziri Mkuu huyo kwamba yeyote aliyehusishwa na ubadhirifu akamatwe na uchunguzi uendelee juu yake.
Nimeipokea Ripoti nyingine kutoka Jeshi la Polisi ambapo watu 12 wanashikiliwa mpaka sasa wakihusishwa na tuhuma za ubadhirifu bandarini Dar es Salaam.
Wahusika hao hawajatajwa majina kwa sababu ya upelelezi unaoendelea, ninayo hapa ripoti ya kituo cha TV ya Channel Ten kuhusu taarifa ya kukamatwa maofisa hao.
Comments
Post a Comment