Posts

Simon Msuva: Kiba anaitendea haki Tanzania

Image
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva ambaye msimu huu ameifungia klabu yake jumla ya mabao 14 amefunguka kwamba, msanii Alikiba anaitendea haki nchi yake ya Tanzania kwa kazi ya muziki ambapo amekuwa akifanya kazi bora zinazoleta sifa kwa nchi. Msuva amesema hayo leo kupitia kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kusema yeye anamkubali sana msanii huyo kutokana na uwezo wake kimuziki na namna anavyoweza kuimba vizuri kila apatapo nafasi. "Kwanza naupenda sana ule wimbo wa wale jamaa wa Kenya wameshirikisha Alikiba 'Unconditionally Bae', naukubali ule wimbo sababu watu wamepangilia sana kazi yao mle ndani na unayasikia kabisa, nimependa mavazi ya mule jinsi walivyovaa ni mavazi fulani ambayo yanawakilisha Afrika japo hata watu wa Ulaya wanavaa lakini naona Afrika watu wanapenda sana kuvaa vile" alisema Msuva Msuva aliendelea kutoa ufafanuzi juu ya wimbo huo na uwezo wa Alikiba "Ukisikiliza ule wimbo unaona jinsi ambavyo Alikiba amefanya vi...

#BREAKING: Wanafunzi wengine watatu wamepoteza maisha leo Geita

Image
Nimeipata hii taarifa kutoka mkoani Geita ikieleza kumetokea ajali ya Mtumbwi ambao ulibeba wanafunzi wa shule ya Ludegea ambapo wanafunzi watatu wamepoteza maisha baada ya kuzama na wengine 21 wamenusurika. Imeelezwa kuwa wanafunzi hao walikuwa njiani kuelekea shuleni wakati ajali ya kuzama mtumbwi huo ilipotokea.

Binti wa miaka 15 abakwa na vijana wanne Jijini Mwanza

Image
    Watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi huku mwingine mmoja akiendelea kutafutwa kwa tuhuma za kumbaka binti mmoja mwenye umri wa miaka 15 wilayani Ilemela, mkoani Mwanza. Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amesema kwamba tukio hilo limetokea tarehe 21/05/2017 majira ya saa moja kamili jioni katika maeneo ya mamlaka ya pamba, kata ya Kirumba ambapo inadaiwa kuwa binti huyo ambaye pia ni mkazi wa Kirumba alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtuhumiwa aliyejulikana kwa jina moja la Phili na walipanga wakutane katika maeneo hayo. Inasemekana kuwa binti huyo alikutana na mpenzi wake mahali hapo kisha walikwenda sehemu yenye jumba bovu kuzungumza, wakiwa kwenye eneo hilo ghafla walitokea vijana wengine watatu wakishirikiana na Phili na kuanza kumfanyia ukatili kwa kumbaka. Inasemekana kuwa wakati wakiendelea na ukatili huo binti alipiga yowe akiomba msaada kutoka kwa wananchi, wananchi walifika eneo la tukio ...

Nimerekodiwa Video ya Ngono Bila Kujijua. Nifanyeje?

Image
    Wadau natumaini mu wazima Mi ni mjasiriamali toka Arusha but huwa nakuja Dar kwa ajili ya kuchukua bidhaa, nikiwa Dar napenda kujibururdisha ama MEEDA au KONA BAA/AMBIANCE AFRIKA SANA huwa nikipata demu wa kupiga nampelekaga Guest/hotel niliyofikia tunafurahia "game" asb namlipa chake anatambaa. Sasa katika kuingia guest kadhaa za hapa Dar nimegundua hawa jamaa wa guest wanaweka SECURITY CAMERAS kuanzia kwenye parking, kwenye korido, karibu na milango, vyumbani hadi bafuni. Je, ni haki kuweka security camera hadi vyumbani/bafuni?     Jana nikiwa kwenye foleni Magomeni Mapipa dogo mmoja akaja na DVD kibao za dini, chini yake ameweka DVD ya X ina picha ya WEMA nikainunua ile kufika hotelini nikaweka kwenye laptop najiona mimi na demu niliyemchukua wk 2 zilizopita.     Hakika nilichoka, sijui cha kufanya nishaurini wadau.

Mwenyekiti wa Tume ya uchunguzi Uvamizi wa Clouds atishiwa Maisha

Image
Mwenyekiti wa Kamati wa Uchunguzi wa Tukio la uvamizi wa kituo cha Habari cha Clouds Televisheni, Deodatus Balile ametishiwa maisha na kudukuliwa mawasiliana. Balile kwenye akaunti yake ya Facebook, ametanabaisha mbinu zilizokuwa zikitumiwa na watu wenye nia ovu naye kwa kudukua mawasiliano yake. Balile ameleeza kuwa mawasiliano hayo yaliingiliwa mpaka kwenye shughuli za Ofisi Balile  pia ni Mkuregenzi Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri "Juzi mawasiliano ya ofisini kwetu yalidukuliwa. Makala inayopaswa kusomwa kesho, waliojiteua kuwa wasaidizi wa aliyetaka nimwombe radhi kwa kufanya kazi niliyotumwa mchana kweupe, wametamba kuwa wanafuatilia maisha yangu hadi uvunguni mwa kitanda changu" amesema Balile. Nimeona nisali kwa sauti sala hii, ili nikipotea, hawa wasaidie kutoa majibu nilipo. Nimeambatanisha baadhi ya meseji zao za udukuzi kwangu.

Npe Amemjibu Makonda, Picha Limeanza Upyaaa

Image
  Siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuhojiwa na kituo cha Star Tv kuhusu mambo kadha wa kadha likiwemo suala la uvamizi wa Clouds Media na kusema Hakupaswa kumuingilia kwakuwa wote ni watumishi... Basi Nape amemjibu hivi... "Niliunda Kamati Kuchunguza TUKIO LA KUVAMIWA KITUO CHA UTANGAZAJI sio kumchunguza RC.Kama RC alikuwa mmoja wa wavamizi, HAYUKO JUU YA SHERIA!‬"

Van Gaal aomba radhi kwa kujiangusha

Image
Van Gaal aomba radhi kwa kujiangusha MANCHESTER, ENGLAND KOCHA wa Manchester United, Van Gaal, ameomba radhi kwa kitendo cha kujiangusha juzi mbele ya mwamuzi wa akiba, Mike Dean, katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal, kwenye Uwanja wa Old Trafford. Kocha huyo alijiangusha kwa makusudi huku akiwa na lengo la kumuonesha mwamuzi jinsi wachezaji wa Arsenal wanavyojiangusha kwa kumdanganya mwamuzi wa mchezo huo. Kocha huyo alimwambia mwamuzi kwamba mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez, amekuwa mjanja hivyo mara kwa mara anajiangusha kwa ajili ya kuomba ili waweze kutumia mipira ya adhabu. Hata hivyo, Van Gaal amekiri kwamba alifanya makosa kuonesha mfano huo mbele ya mashabiki ambao walionekana kushangilia. “Halikuwa jambo zuri kufanya mbele ya mwamuzi wa kati, mshika kibendera na mwamuzi wa akiba, ninakubali kwamba nilifanya makosa na natumia muda huu kuomba radhi kwa kitendo ambacho nilikifanya, japokuwa mashabiki walionekana kuf...