Mwenyekiti wa Tume ya uchunguzi Uvamizi wa Clouds atishiwa Maisha
Mwenyekiti wa Kamati wa Uchunguzi wa Tukio la uvamizi wa kituo cha Habari cha Clouds Televisheni, Deodatus Balile ametishiwa maisha na kudukuliwa mawasiliana.
Balile kwenye akaunti yake ya Facebook, ametanabaisha mbinu zilizokuwa zikitumiwa na watu wenye nia ovu naye kwa kudukua mawasiliano yake.
Balile ameleeza kuwa mawasiliano hayo yaliingiliwa mpaka kwenye shughuli za Ofisi
Balile pia ni Mkuregenzi Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri
"Juzi mawasiliano ya ofisini kwetu yalidukuliwa. Makala inayopaswa kusomwa kesho, waliojiteua kuwa wasaidizi wa aliyetaka nimwombe radhi kwa kufanya kazi niliyotumwa mchana kweupe, wametamba kuwa wanafuatilia maisha yangu hadi uvunguni mwa kitanda changu" amesema Balile.
Nimeona nisali kwa sauti sala hii, ili nikipotea, hawa wasaidie kutoa majibu nilipo. Nimeambatanisha baadhi ya meseji zao za udukuzi kwangu.
Comments
Post a Comment