Will Smith kususia tuzo za Oscars
Msanii wa Filamu
Will Smith amethibitisha kwamba ataungana na mkewe, Jada Pinkett Smith,
katika kususia tuzo la Oscars mwezi ujao.
" Hatujihisi vizuri kusimama huko na kusema hii ni sawa,"alimueleza mtangazaji wa kipindi cha Good Morning America Robin Roberts.
Msanii wa vichekesho Chris Rock anakabiliwana miito ya kumtaka ajiondoe kwenye kazi aliyopewa kama mwongozaji wa taratibu za tuzo la Oscas mwaka huu, huku mzozo huo ukiendelea.
Katika mahojiano yaliyotangazwa Alhamisi Smith alisema uteuzi wa mwaka huu ulizingatia "wamarekani wenye mamlaka" na kwa hilo , "kwa kiwango kikubwa , Hollywood iliunda sura ya kufikirika ya uzuru".
Alipoangalia orodha nzima iliyojaa wazungu pekee walioteuliwa kuwania ushindi wa Oscars, aliendelea kusema, "haikuonyesha dhahiri uzuri huo ."
Katika mahojiano yaliyotangazwa Alhamisi Smith alisema uteuzi wa mwaka huu ulizingatia "wamarekani wenye mamlaka" na kwa hilo , "kwa kiwango kikubwa , Hollywood ilibuni sura ya kufikirika ya uzuru".
Alipoangalia orodha nzima iliyojaa wazungu pekee walioteuliwa kuwania ushindi wa Oscars, aliendelea kusema, "haikuonyesha dhahiri uzuri huo ."
Baadhi walitarajia Smith, mtu alieteuliwa mara mbili kwa tuzo hilo, kuorodheshwa tena ,kwa filamu ya Concussion ambapo alicheza kama daktari aliechunguza majeraha ya kichwa ya wachezaji soka wa Marekani.
Comments
Post a Comment