JINSI YA KUJITIBU UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME-2-3

Wiki iliyopita tuliianza mada hii ya kujitibu nguvu za kiume ambapo tuliweza kufahamu mfumo wa uzazi wa mwanaume, tuendelee kujifunza somo hili.
Kuna viungo vya ndani, kiungo kkimoja inaitwa seminal vessel, seminal vessel ni kama tezi mbili ambazo kazi yake ni kuzalisha majimaji yanayokwenda kuungana na majimaji yanayozalishwa kwenye protest grand ambayo yanaitwa semen ambazo kazi yake ni kuzibeba mbegu za uzazi za mwanaume ambazo kitaalamu zinaitwa sperm.
Pia kuna kiungo kingine kinaitwa prostate grand, hii ni tezi ya prostate na watu wengine wanaiita tezi dume au tezi ya mwanaume. Tezi hii ipo karibu kabisa na kibofu cha mkojo, kwani nyuma ya tezi hii imeungana na kibofu cha mkojo, prostate grand kazi yake ni kuzalisha seminal fluid ambazo huungana na majimaji yanayozalishwa kwenye seminal vessel kwa ajili ya kutengeneza semen.
Kuna kiungo kingine kinaitwa capas grand hizi ni kama mbegu mbili ambazo hukaa pamoja, nazo huzalisha majimaji mengine ambayo huwa yanaingia kwenye njia ya mkojo (urethra) na kazi yake huwa ni kuandaa mfereji wa mkojo kupitisha mbegu za mwanaume.
Hii ni kwa sababu mwanaume akipata haja ndogo huwa kuna mabaki ya mkojo kwenye njia ya mkojo (urethra) ambayo yana asili ya asidi (acid) na ndiyo maana zikawepo hizi capas grand ambazo hutengeneza majimaji ambayo yanaenda kusafisha ile asidi kwenye njia ya mkojo yenye asili ya alkaline ili kuweka hali ya usafirishaji mzuri wa mbegu za mwanaume.
Pia kuna kiungo kingine kinaitwa ejaculatory duct, ejaculatory duct ni sehemu ya mwisho kabisa baada ya kuungana na vas deferens inayotokea kwenye korodani na kuungana na mrija unaotoka kwenye kibofu cha mkojo kwenda kwenye prostate grand.
Mwanzo kwenye prostate grand kuna kiungo kinaitwa ejaculatory duct ambapo huwa panatoa msisimko wa mtu kuweza kutoa mbegu wakati wa tendo la ndoa, hizi zimetengenezwa kwenye prostate grand, zilizotengenezwa kwenye seminal vessel, mbegu zinazotengenezwa kwenye korodani na kuhifadhiwa kwenye epididymis zikaletwa na vas deferens kwenda pale kwenye prostate grand na kutolewa nje.
Comments
Post a Comment