ALIKIBA AMEAHIDI KUACHIA VIDEO NYINGINE MPYA >>>BAADA YA NAGHARAMIA KUFIKISHA VIEWERS MILIONI MOJA,>> SOMA ZAIDI HAPA>>

http://nyotanjema.blogspot.com/

Hakuna kitu kizuri kama ukiona kile unachokifanya kinawapendeza wengi, jambo hili hupelekea kuongeza jitihada katika kile unachokifanya ili uendelee kufanya vyema maradufu na pongezi zizidi kuendelea kwa kukurejeshea au kukuongezea heshima yako kwa kile unachokifanya

Hivi ndivyo msanii Alikiba anavyofurahia kuona watu wanapenda na kuunga mkono kila anachokifanya, hii inatokana na kazi nzuri aliyofanya na msanii mwenzake Christian Bela inayoitwa Nagharamia ambayo hivi sasa imetimiza viewers Milioni moja kwa muda wa wiki nne tangu kuachiwa kwake.

Jambo hilo limempelekea Alikiba kuwaahidi mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa baada ya video hiyo kutimiza viewers Milioni moja anataraji kuachia video yake mpya hivi karibuni,ambapo kwa tetesi zinasema kuwa video ya nyimbo hiyo inaitwa Lupela aliyofanyia nje ya nchi.

Comments

Popular posts from this blog

TAZAMA PICHA 30 ZA MREMBO AGNES MASOGANGE AKIJIACHIA KISTAA NJE YA NCHI

Gamboshi: Makao Makuu ya Uchawi na Wachawi yaliyopo Shinyanga, Tanzania

14 parties want Parliament to discuss Zanzibar impasse