WHERE IS CCM? (CCM IKO WAPI?)
WHERE IS CCM? (CCM IKO WAPI?)
Rafiki yangu mmoja leo amenivunja mbavu , ananiambia juzi alimpigia simu kiongozi mmoja wa juu wa CCM ambaye wakati wa kampeni alikuwa ni kati ha watu 50 muhimu waliosimamia, kupigania na kulinda ushindi wa Magufuli (achilia mbali utata wa ushindi huo, hâta hivyo kikatiba tayari Magufuli ni Rais).
Simu ile ilikuwa kutaka kujua maoni ya mwana CCM huyo nguli juu ya KASI YA UTENDAJI WA MAGUFULI na kwamba CCM inafarijika kwa kiasi gani. Jibu alilopewa mwandishi ni "NO COMMENT...", kwamba mwana CCM huyu aliyempigania Magufuli, hana maoni juu ya utendaji wa siku 22 za awali.

Kisa hiki kikanipa tafakari muhimu sana siku ya leo, kwamba mbona hatuoni matamko mazito ya taasisi na ngazi za uongozi ndani ya CCM kusifia kwa uwazi hatua za bosi wao? Mbona sioni UVCCM, UWT, lile baraza la wazee la CCM na ile Idara ya vyuo vikuu? Mbona sioni pilikapilika za CCM kama chama kujawa na furaha kubwa sana? Kuna nini?
Mara kadhaa nimeona mwana CCM mmoja mmoja akitoa katamko kake hapa Facebook kusifia utendaji wa Magufuli, sijaona CCM kama chama tena chini ya Mwenyekiti wake JK kikisimama hadharani kupongeza, kuunga mkono na kutangaza rasmi kuwa KIMBIZA KIMBIZA hii ya Magufuli ndiyo hasa chama kiliisubiri.
Niliambiwa Mwenyekiti wa CCM yuko Ethiopia, huwenda akirudi atatoa tamko zito la kuunga mkono juhudi hizi, maana yule Rais wetu mstaafu ni muungwana na mtu asiye na makuu.
Ukianza kuona CCM inapata kigugumizi kusimama hadharani kupigana upande wa Rais wake, ujue basi WANAISOMA NAMBA. Na wale wenzangu na mimi waliodhani kuwa sijui upinzani utaisoma namba, warudi walitizame hili tena, liko kinyume.
Jambo hili linanifanya nianze kuona kuwa kumbe wengi wa wana CCM na vigogo wa CCM walimpigania Magufuli abakie madarakani si kwa lengo la kuleta mabadiliko bali ilikuwa ni kwa uhakika kuwa CCM itaendelea kuwepo kwenye dola na mirija yote ya wizi na ma DEAL makubwa vitapotea.
Wana CCM wengi huwenda waliamini katika kuendelea kuongoza dola kwa lengo lile lile la kutafuna pesa, kujenga ukuu n.k. Sijui kama kati yao hâta kuna asilimia kumi walidhani kuwa mambo yatakuwa TOO SERIOUS like what it seems to be!
Kama ni kuisoma namba, basi itasomwa humo CCM ndani kwa ndani. Na ikisomwa huku nje itawahusu mafisadi na matajiri wanaoifadhili CCM usiku na mchana, ita BACK FIRE kwa CCM yenyewe.
Sisi wengine ambao hatukuwahi kuishi kwa kutegemea NETWORK za CCM wala fadhila za vyeo, mali n.k. tuna amani télé mioyoni mwetu, hofu ni kwenu ninyi wenzetu.
JITEGEME KIMAWAZO.COM

Comments
Post a Comment