Posts

Showing posts from December, 2015

Serikali Yasema Haijengi Nyumba za Kuwapa Wananchi Bure

Image
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula       SERIKALI imesema kuwa haina mpango wakujenga nyumba za kuwapa Wananchi bure kutokana na gharama ambazo Serikali inagharamia katika ujenzi nyumba hizo. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula (Pichani)wakati alipotembelea Shirika la Nyumba la Taifa(NHC). Angeline amesema kuwa shirika la nyumba la Taifa linajenga nyumba kwaajili ya kuuzwa pamoja na kupangisha na si kuwapa wanchi bure. Amesema kuwa gharama ya kujenga nyumba hizo inakuja katika maandalizi ya ujenzi ikiwa ni pamoja na kuandaa miundombinu kama Barabara, Maji pamoja na Umeme. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC), Nehemia Mchechu amesema shirika hilo tayari limejenga nyumba za kutosha katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Arusha na Mwanza. Pia amesema katika nyumba za mikoani shirika hilo limeuza nyumba hizo kwa 40% hadi 50% huku akisi...

Lipumba .Asema Mgogoro Utakwisha Iwapo Dr Shein Atakubali ZEC Iendelee Kutangaza Matokeo

Image
      Mwenyekiti wa zamani wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba     Mwenyekiti wa zamani wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ndiye mtu pekee mwenye uwezo wa kumaliza mgogoro wa Zanzibar. Akizungumza Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema mgogoro wa Zanzibar utamalizwa kwa Dk Shein kuiruhusu Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25. Alisema pamoja na mazungumzo yanayoendelea kati ya CUF na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk Shein ndiye mwenye uwezo kuumaliza mgogoro huo. “Mazungumzo yanaendelea na hatujui yatafika mwisho lini, lakini Dk Shein ndiye anayeweza kuifanya Zanzibar iwe na amani au vurugu, ninashauri aruhusu kutangazwa kwa matokeo,” alisema. Alisema amani na utulivu uliopo Zanzibar wakati wananchi wakisubiri hatima ya mgogoro huo, haiwezi kuwa ya kudumu kwani ikiamuliwa uchaguzi urudiwe wapo ambao hawatakubali. Profesa Lipumba alisem...

Kamanda Suleiman Kova Astaafu Rasmi Jeshi la Polisi Tanzania!

Image
Leo ni siku ya mwisho kwa Kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova, kulitumika jeshi la Polisi nchini kwa kuwa muda wake wa kulifanyia kazi jeshi hilo umeisha. Kamanda Kova ametoa taarifa hiyo leo asubuhi alipokuwa akizungumza katika kipindi cha kumekucha cha ITV, na kusema kuwa mkataba wake na jeshi la Polisi umeishia leo, hivyo analazimika kukaa pembeni. "Mmepata bahati sana, maana wakati nakuja Dar es salaam mwaka 2008 nikitokea Mbeya, kwa mara ya kwanza nilifanya kipindi hapa na leo hii nawaagia hapa, leo ndio siku ya mwisho kwangu kulitumikia jeshi la Polisi, mkataba wangu na jeshi la Polisi unaisha leo, lakini siwaachi hivi hivi, Kaimu wangu yupo atakuwa nanyi", alisema Kamanda Kova. Kamanda Kova alikuwa Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es salaam, na kwa mujibu wake amefanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa matukio ya kiuhalifu, yaliyokuwa yanaitikisa nchi hususani matukio ya wizi na uvamizi wa kwenye benki.

CUF Yatoa Tamko >>>>>>>>>>>Kutoshiriki Sherehe za Mapinduzi Zanzibar....Tamko Zima Liko Hapa

Image
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI   Tokea yalipofanyika Mapinduzi ya tarehe 12 Januari, 1964, tumekuwa tukiadhimisha tukio hilo kubwa katika historia ya Zanzibar kila mwaka inapofika siku hiyo.  Tukio hilo kubwa ndilo lililopelekea kutangazwa kwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume. Chama Cha Wananchi (CUF) kimekuwa kikishiriki kikamilifu katika maadhimisho ya siku hiyo kila mwaka kwa kutambua kwamba Mapinduzi ya tarehe 12 Januari, 1964 ni Mapinduzi ya Wazanzibari wote.  Malengo makuu ya Mapinduzi hayo yameelezwa na kufafanuliwa vyema kupitia Dikrii Nam. 6 ya mwaka 1964 iliyopitishwa na Baraza la Mapinduzi ambayo yanatajwa kwamba ni kuleta usawa, umoja na maridhiano baina ya Wazanzibari wote na kupiga vita aina zote za ubaguzi. Tayari tumetangaziwa kwamba kuanzia tarehe 2 Januari, 2016 kutakuwa na shughuli mbali mbali zenye lengo la kuadhimisha Mapinduzi yetu na hatimaye, kama ilivyo ada na desturi, kufik...

Billnass+ft+TID+++Ligi+Ndogo+%28+Official+Music+Video Download Free now

Image
finished the year well to quench your eyes and minds to see new video DOWNLOAD VIDEO free now

Rais mstaafu Kikwete, Waziri Lwenge wakagua mitambo ya maji Wami, Chalinze

Image
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (katikati), akizungumza na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge wakielekea kukagua mitambo ya kusafisha na kusafirisha maji Wami, katika Halmashauri ya Mji wa Chalinze, mkoani Pwani, Desemba 30, 2015. Rais Jakaya Kikwete na Lwenge wakiangalia mitambo ya kusafisha maji     Wakiwa katika picha ya pamoja       Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete , akizungumza na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge (kushoto kwake) wakielekea kukagua mitambo ya kusafisha na kusafirisha maji Wami, katika Halmashauri ya Mji wa Chalinze, mkoani Pwani jana.Wa pili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete.     Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akionesha kitu walipotembelea mitambo ya maji Wami       Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge katika mitambo hiyo.

Nafasi MPYA Kabisa>>>>Profesa Joyce Ndalichako na siyo "Dokta" tena

Image
  WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, imefafanua kuwa sifa ya kitaaluma ya waziri wa wizara hiyo ni Profesa Joyce Ndalichako; na siyo Dk Joyce Ndalichako. Taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam juzi na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha wizara hiyo, ilisema tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo wiki iliyopita, kwa bahati mbaya sifa ya kitaaluma ya waziri huyo, imeendelea kujulikana kama Dokta. “Tunapenda kuufahamisha umma kwamba cheo cha kitaaluma cha Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Dokta Joyce Ndalichako kwa sasa ni Profesa Joyce Ndalichako”, ilisisitiza taarifa hiyo ya wizara Taarifa hiyo ilisema wafanyakazi wa wizara hiyo, wanampongeza waziri kwa uteuzi huo na wanaahidi kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake kwa weledi na uadilifu katika kuendeleza sekta ya elimu na mafunzo nchini

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Tarehe 31 Disemba>>>> Kubwa Zaidi Ni Makufulia Awateuwa Makatibu Wakuu

Image

Jeshi la Polisi lafumuliwa

Image
  nspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu amelifumua Jeshi la Polisi nchini kwa kupanga na kupangua vigogo wake, huku baadhi wakipandishwa nyadhifa.... read more...

New Audio : MAE Music ft Dully Sykes - Kitopokolo.....Listen & Download.

Image

Vitendawili 8 kwa Magufuli Zanzibar Imetolewa 28/12/2015

Image
Rais Dk. John Magufuli  Na Gwamaka Alipipi  Wakati Rais Dk. John Magufuli, akikutana kwa nyakati tofauti na waliokuwa wagombea urais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Maalim Seif Sharif Hamad, wa Chama cha Wananchi (CUF), imefahamika kuwa Rais huyo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anakabiliwa na vitendawili takriban nane kuhusiana na hatma ya kisiasa kwenye visiwa hivyo.   Uchunguzi uliofanywa na Nipashe kwa kuhusisha mahojiano na wachambuzi kadhaa wa masuala ya siasa nchini umebainisha kuwa baadhi ya vitendawili hivyo vinavyotokana na mustakabali wa Zanzibar baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa visiwa hivyo uliofanyika Oktoba 25, 2015 ni pamoja na kujua ni vitu gani ambavyo Dk. Shein (CCM) na Maalim Seif (CUF) watakubali kuvipata au kuvipoteza baada ya kupatikana kwa suluhu ya mgogoro uliopo sasa. Uchaguzi ulifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, aliyeitaja...

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya Disemba 29>>>> Kubwa Zaidi ni MAALIM SEIF vs CCM SITA

Image