Real Madrid wafuta machungu ya El Clasico kwa kuifunga Eibar, haya ndio matokeo kamili (+Pichaz&Video)

Baada ya Jumamosi ya November 28 klabu ya FC Barcelona kushuka dimbani kucheza mchezo wake 13 dhidi ya Real Sociedad na kuibuka na ushindi wa goli 4-0, November 29 ilikuwa zamu ya wapinzani wao wa jadi klabu ya Real Madrid ya Hispania ambao wao walilazimika kusafiri hadi dimba la Municipal de Ipurúa kucheza na klabu ya Eibar.
takashi-inui-eibar-toni-kroos-real-madrid
Real Madrid ambayo ilikuwa ugenini na wachezaji wake nyota kama Cristiano Ronaldo na Gareth Bale ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya wenyeji wao klabu ya Eibar, licha ya kuwa Real Madrid hawana kumbukukumbu nzuri katika mchezo wao wa El Clasico uliyochezwa weekend iliyopita, ilifanikiwa kuondoka na point 3 na kufanya tofauti yake na FC Barcelona kuwa ya point 6.
2EE80D3700000578-0-image-a-68_1448815339773
Hata hivyo ushindi walioupata Real Madrid haukuwa mwepesi kwani klabu ya Eibar ilikuwa imefanikiwa kuwadhibiti Real Madrid hadi dakika ya 43 ndio Gareth Bale akafanikiwa kufunga goli la kwanza, goli la pili la Real Madrid lilifungwa kwa mkwaju wa penati na nyota wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu hiyo Cristiano Ronaldo dakika ya 82.
Video ya magoli ya Eibar Vs Real Madrid November 29.

Comments

Popular posts from this blog

TAZAMA PICHA 30 ZA MREMBO AGNES MASOGANGE AKIJIACHIA KISTAA NJE YA NCHI

Gamboshi: Makao Makuu ya Uchawi na Wachawi yaliyopo Shinyanga, Tanzania

14 parties want Parliament to discuss Zanzibar impasse