Don Jazzy na watu wake wa Mavins wamejikusanya kuileta mpya yao >> ‘JantaJanta’- Video
Don Jazzy alianza safari ya muziki akiwa na D’Banj miaka mingi iliyopita, wakaibeba vizuri bendera ya Nigeria na kuifanya Dunia ikajua nguvu ya Nigeria kwenye muziki… lakini wakaona kuna umuhimu kuwabeba na wengine nao watambulike duniani kupitia muziki.
Hiyo ilifanya milango kufunguka kwa mastaa wengine kibao ikiwemo akina Tiwa Savage, Dr SID, D’Prince, Reekado Banks, Korede Bello na mrembo Di’Ja.
Usipitwe na kitu kipya kutoka crew nzima ya Supreme Mavin Dynasty ikiongozwa na Don Jazzy mwenyewe… wimbo unaitwa ‘JantaJanta‘, utaweza kuhit na kugusa level za Dorrobucci?

Comments
Post a Comment