Posts

Showing posts from March, 2016

Van Gaal aomba radhi kwa kujiangusha

Image
Van Gaal aomba radhi kwa kujiangusha MANCHESTER, ENGLAND KOCHA wa Manchester United, Van Gaal, ameomba radhi kwa kitendo cha kujiangusha juzi mbele ya mwamuzi wa akiba, Mike Dean, katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal, kwenye Uwanja wa Old Trafford. Kocha huyo alijiangusha kwa makusudi huku akiwa na lengo la kumuonesha mwamuzi jinsi wachezaji wa Arsenal wanavyojiangusha kwa kumdanganya mwamuzi wa mchezo huo. Kocha huyo alimwambia mwamuzi kwamba mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez, amekuwa mjanja hivyo mara kwa mara anajiangusha kwa ajili ya kuomba ili waweze kutumia mipira ya adhabu. Hata hivyo, Van Gaal amekiri kwamba alifanya makosa kuonesha mfano huo mbele ya mashabiki ambao walionekana kushangilia. “Halikuwa jambo zuri kufanya mbele ya mwamuzi wa kati, mshika kibendera na mwamuzi wa akiba, ninakubali kwamba nilifanya makosa na natumia muda huu kuomba radhi kwa kitendo ambacho nilikifanya, japokuwa mashabiki walionekana kuf...

Wenger ashitushwa na kiwango cha Rashford

Image
MANCHESTER, ENGLAND KOCHA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger, amedai kwamba ameshitushwa na uwezo wa nyota wa Manchester United, Marcus Rashford, aliouonesha juzi katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 18, juzi alionesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo huo dhidi ya Arsenal, ambapo alipachika mabao mawili ndani ya dakika tano katika kipindi cha kwanza kwenye ushindi wa mabao 3-2. Kutokana na kiwango hicho, Wenger amedai kwamba hakutarajia kuona uwezo mkubwa ambao aliuonesha mchezaji huyo. “Kwa upande wetu, tulishindwa kuwa na mipango mizuri ya kutafuta mabao kutokana na nafasi ambazo tulizipata, lakini katika mchezo huo nilikuja kushangazwa na uwezo wa nyota mpya wa Man United, Rashford. “Nadhani haikuwa kwangu tu, ilikuwa kwa kila mmoja kushangazwa na uwezo wa mchezaji huyo ambaye alifanikiwa kufunga mabao mawili, alikuwa na akili ya kwenda na mchezo na kujua wapi sehemu sahihi ya kukaa. “Ninaamini atakuja kuwa na u...

*Mdee, Kubenea wakamatwa, Simbachawene atoa neno>>>>Mahakama yakana kuzuia uchaguzi wa Meya Dar Soma Zaidi Hapa>>>>>

Image
Hakimu: Zuio umeya Dar feki *Mdee, Kubenea wakamatwa, Simbachawene neno NA WAANDISHI WETU, DAR ES SALAAM MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema hakuna amri iliyotolewa kuzuia Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliotakiwa kufanyika Februari 26, mwaka huu. Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Waliarwande Lema, alisema hayo jana alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu amri hiyo aliyodaiwa kuito kuzuia uchaguzi huo. “Hakuna amri ya kuzuia uchaguzi wa meya, aliyesema mahakama imetoa zuio ni muongo,” alisema Hakimu Lema. HAKIMU MFAWIDHI KISUTU Awali mapema asubuhi jana, waandishi wa habari za mahakama waliwasili ofisini kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Cysprian Mkeha kutaka ufafanuzi kuhusu zuio linalodaiwa kutolewa na mahakama hiyo kuzuia uchaguzi huo wa meya. Hakimu Mkeha, alisema Februari 25, mwaka huu hadi anaondoka kazini hakukuwa na maombi yoyote yaliyowasilishwa kupinga Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam. Alisema ...

YAJUE MAMPYA YALIO JIRI KATIKA MAGAZETI YA LEO Juma Nne March 1>>>SOMA ZAIDI HAPA>>>

Image

Halima Mdee Atupwa Rumande......Mahakama yakana kuzuia uchaguzi wa Meya Dar

Image
Wakati mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee akilala rumande akihusishwa na vurugu zilizotokea Jumapili wakati uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam ulipokwama, Mahakama ya Kisutu imelikana zuio lililotumika kuzuia shughuli hizo.  Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Januari 23, mwaka huu, lakini uliahirishwa ili kuandaa mfumo bora wa upatikanaji wajumbe kutokana na CCM kutaka kuingiza wapigakura nje ya waliotakiwa. Ulikwama tena Februari 8, baada ya Halmashauri ya Jiji la Dar kubaini kasoro ya nyongeza ya majina 14 ya wajumbe kutoka manispaa za Ilala na Kinondoni. Jumapili iliyopita ilikuwa ni mara ya tatu, kukwama tena kutokana na zuio lililosababishwa na kesi iliyofungiliwa na Saad Kimji na Suzan Masawe. Hata hivyo, zuio hilo la muda la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu lililotumika kuahirisha uchaguzi wa meya na naibu meya wa Jiji, uliopaswa kufanyika Februari 27, 2016 limebainika kuwa ni batili. Jana, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu,...

CCM JOTO LAPANDA Wasaliti’ waanza kutumbuliwa bila ganzi

Image
Wasaliti’ CCM waanza kutumbuliwa bila ganzi Huku kukiwa na taarifa kuwa wasaliti wa CCM wanaotarajiwa kutimuliwa wengi ni watu maarufu hasa viongozi wa ngazi za mkoa, tayari viongozi 21 wa Manyara, wameshatumbuliwa majipu bila ganzi. Jumla ya viongozi 21, watatu wakiwa ni wa CCM Wilaya ya Babati Mjini mkoani Manyara na wengine 18 wa ngazi ya kata, wameshaadhibiwa na Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete alichokiita kutumbua majipu bila aibu. Inadaiwa kuwa viongozi hao walikuwa wanamshabikia aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa. Imedaiwa ushabiki ulisababisha CCM ipoteze jimbo na kata tano kati ya nane za Babati Mjini. Katibu wa CCM mkoani Manyara, Ndeng’aso Ndekubali aliwataja waliofukuzwa uanachama kuwa ni wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa, Cosmas Masauda, Zulekha Mohamed na mjumbe wa mkoa, Felix Kivuyo. “Hawa wamefutwa uanachama baada ya kudaiwa kukisaliti chama kwa kuwapigia kampeni wagombea wa vyama vya upinzani na kuwaombea kura kwenye Uchaguzi...