JIANDAE NA HILI>>>> BARAKA DA PRINCE, JAY MOE KUJA NA KOLABO MATATA
Msanii anayefanya vyema na wimbo wa Nivumilie alioshirikiana na Rubby, Baraka Da Prince, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka picha akiwa studio na wakongwe wa muziki nchini akiwemo mtayarishaji wa muziki P Funk Majani wa Bongo Record na Jay Moe

Katika picha hiyo Baraka Da Prince aliandika ujumbe wa kuashiria kuwa wamerekodi wimbo, hivyo hivyo kwenye ukurasa wa msanii Jay Moe ameweka picha wakiwa pamoja na kusifia alichokifanya Baraka Da Prince katika wimbo huo ambao hawajabainisha ni upi, jambo lililopelekea mashabiki kusifu hatua hiyo.

kaka lini hiyo yaja?
ReplyDeleteSIKU SIO NYINGI SANA mambombo yakuwa yame kamilika
ReplyDelete