RAY C AJITOLEA KUMSAIDIA DAZ BABA KUACHA MADAWA YA KULEVYA
Staa wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameapa kumsaidia mwanamuziki mwenzake David Jacob ‘Daz Baba’ anayedaiwa kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya.
Chanzo cha kuaminika kimeeleza kuwa, Ray C amekuwa akiumizwa na hali aliyonayo Daz Baba na amefanya kila awezavyo hadi kuongea naye ili aanze kutumia dozi ya Methadone ambayo wengi huipata katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar.
“Ni kweli hali ya Daz Baba inasikitisha na Ray C huyuhuyu unayemjua kaongea naye na amemshawishi kuanza kutumia dozi,” kilidai chanzo hicho ambacho ni rafiki wa Ray C.
Baada ya kuzipata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Ray C, alipopatikana alikiri kuanza mazungumzo na Daz ila akaomba asizungumzie walipofikia kwa sasa.
Comments
Post a Comment