Kuna uwezekano wa Will Smith kuingia kwenye Siasa? Hii ndio mipango yake ya badaaye…
Mkali wa kuigiza movie kutoka Hollywood , Will Smith anafahamika kama mmoja ya wasanii wakubwa sana duniani, ukiachia hayo Will Smith amejijengia jina kubwa sana kwenye muziki kama rapper lakini nini kinaendelea kichwani mwa staa huyo kuhusu maisha yake ya badaaye? Nimekutana na interview aliyofanya Will Smith na The Hollywood Reporter siku chache zilizopita na humo Will amegusia ndoto za kuingia kwenye siasa miaka ya karibuni >>> “ Sipendi kukaa sehemu moja kwa muda mrefu, kwahiyo nahisi mpaka hapa nilipofikia naendelea kukuza uwezo wangu wa kutoa mchango wangu duniani… nimepitia vitu vingi kwenye kila kitu nilichokigusa kwenye safari yangu na inafika wakati unaona inabidi uendelee kuiandika stori yako kwa kuangalia majukwaa mengine yanayoweza kutoa kile kilicho ndani yako na kushare na wengine… nikilitazama dirisha la siasa naona kuna uwezekano wa mimi kuwa na future nzuri tu huko. Wanaweza wakanihitaji siku moja kutumia sauti yangu na mawazo niliyonayo… ” <...