Posts

Kijana: Ukipenda Jimama au Mwanamke Mwenye Pesa Uvumilie Vipigo/Kugombezwa Hadharani

Image
Wale vijana wenzangu mnaopenda majimama (kulelewa) mkubali makofi, makonzi sometimes mitama hadharani, pia hata kufokewa hadharani. Maana wengi wa hawa majimama wana stress za kutosha lakini usisahau ndo yanayowaweka baadhi ya vijana mjini kwa kila kitu, la muhimu ukishagombezwa we jidai kujichekesha tu ili mambo yaishe. Pia nawasihi sana baadhi vijana tusiwapende hawa majimama tutafute maisha yetu, tusipende maisha ya bure kwani tunaweza kupata madhara mengi ikiwemo magonjwa UKIMWI na kukosa vijana wa kujenga taifa.

Johari Akiri Kumpora Kimapenzi Mwigizaji Ray Kutoka kwa Mainda

Image
STAA wa sinema za Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amekiri kwamba wakati anaingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na nyota wa fani hiyo, Vincent Kigosi ‘Ray’ alijua yupo na nguli wa filamu, Ruth Suka ‘Mainda’, Johari Amekiri Baada ya kuulizwa na Gazeti moja maarufu ....

Jack Patrick Aandika Barua Akiwa Gerezani Kuhusu Mapenzi ya Diamond na Zari , Vanessa na Jux na Aunty na Iyobo

Image
Wakati akiendelea kutumikia kifungo akiwa jela huko Macau, Hong Kong nchini China, modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff  ‘Jack Patrick’ amenena mazito juu ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Juma Khalid ‘Jux’, Vanessa Mdee, Aunt Ezekiel na Moze Iyobo. BARUA KUTOKA CHINA Jack aliyekamatwa nchini humo kwa msala wa madawa ya kulevya ‘unga’ mwaka 2013 kisha kufungwa miaka sita kwenye Gereza la Macau, hivi karibuni alilitumia gazeti hili barua nzito akionesha kushtushwa na vitu fulani vya mastaa hao. MIMBA YA AUNT Moja kati ya mambo yaliyomshtua Jack ni mimba ya mwigizaji Aunt Ezekiel ambaye ni mke wa mtu, Sunday Demonte anayodaiwa kupachikwa na mcheza shoo wa Diamond, Moze Iyobo. Hata hivyo, katika skendo hiyo, Jack aliwataka watu wamuache Aunt apumzike kwani mapenzi hayachagui hasa kama ana furaha. “Nimeshtushwa na udaku special Lol! Sasa Aunt ameamua kutulia na Iyobo…acha apumzike mapenzi hayachagui as long a...

Mrembo Huddah Monroe Asema Kazi yake ya Kuwapa Raha Wanaume Inalipa..Aonyesha Kadi ya Range Rover Analomiliki

Image
Mrembo Huddah Monroe Mrembo wa Kenya Huddah Monroe Amejitokeza na kuwaponda wale waandishi wa Habari Bloggers wanaosema gari aina la Range Rover analoendesha kwa sasa ameazima kwa mtu na kusema kuwa kazi anayofanya (Socialite ) ya Kutoa Escort kwa kuwapa raha wanaume na kuhuzuria events mbali mbali inamlipa sana kiasi hawezi azima gari ...Huddah Ameweka Mtandaoni kadi ya gari hiyo ambalo ni la gharama sana kwa mtu wa kawaida ikionyesha jina lake halisi kama mmiliki halali wa Ndinga hiyo matata Kadi ya Gari aina ya Ronger Rover ikionyesha jina halisi la Huddah

Diamond, Ommy Dimpoz, January na wengine walaani mauaji ya albino

Image
Mauaji ya mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja, Yohana Bahati huko Chato yamewaumiza watu wengi si Tanzania tu bali dunia nzima. Kifo cha kusikitisha cha mtoto huyo aliyekutwa amekatwa miguu na mikono kimeandikwa na mashirika yote makubwa ya habari duniani na hivyo kuipa Tanzania sifa mbaya. Wananchi wamelaani vikali kitendo hicho na kuitaka serikali kuchukua hatua kuhakikisha haviendelei tena. Hivi ndivyo mastaa wa Tanzania nao walivyoungana na wananchi wengine kueleza waliyonayo moyoni. Diamond Ndugu zangu! nafkiri ni Muda wa kubadilika sasa…Tuacheni fikra potofu, za Kipuuzi na ukatili Usio na Maana.. Hivi inamaa unataka kuniambia na hao kina Bill gates Mzee wa kuku, Carlos Slim, Amancio Ortega , Bakhresa na Matajiri wakubwa Duniani pia Walitajirika kupitia Ukatilii huu wa Ma Albino…??? Juhudi na Utendaji wako wa Kazi ndio utao kufanya Uendelee na kufikia Hayo Malengo unayoyataka… Tuache kujidanganya na Kuwatesa Ndugu zetu wasio na Hatia. Ommy Dimpoz Tanzania inazidi kupata sif...

Picha: Huddah Monroe Achefua Tena Watu Mtandaoni, Atupia Picha Akiwa Mtupu Kitandani

Image
Huddah Monroe ameshajikubali kuwa ni ‘good girl gone bad’ na ndio maana haoni tatizo kuweka picha akiwa kitandani kama alivyozaliwa. Mrembo huyo wa Kenya amepost picha kwenye akaunti yake ya Facebook akiwa kitandani huku akiwa amejifunika na shuka sehemu ndogo tu ya mwili wake kuficha sehemu ny*ti. Mashabiki wake hawakusita kumchana.

FAMILIA, POLISI NA KANISA WAMTENGA ASKARI ALIYEJIUA KWA RISASI MDOMONI....AZIKWA BILA HUDUMA ZA KIDINI WALA KIJESHI

Image
Polisi aliyejiua kwa kujipiga risasi mdomoni, Aloyce Mafuru (24), amezikwa katika makaburi ya Mugumu, Wilaya ya Serengeti, Mkoa wa Mara bila huduma za kidini na kijeshi. Askari huyo aliyekuwa dereva wa Kamanda wa Polisi Wilaya ya Manyoni, Alute Makita alijiua Februari 2 nyumbani kwake na kuacha ujumbe kuwa polisi wasiangike kufanya uchunguzi kwani huo ni uamuzi wake binafsi. Paroko wa Kanisa Katoliki Mugumu, Padri Aloyce Magabe jana aliwaeleza waombolezaji kuwa ingawa Mafuru alipata kipaimara, lakini kujiua kumesababisha kanisa kushindwa kuendesha ibada ya mazishi kwa kuwa kitendo hicho siyo mapenzi ya Mungu. “Haifai kusema bwana ametoa na bwana ametwaa, maana tendo alilofanya huyu  halimtukuzi Mungu bali shetani, maana ni kama ilivyofanyika kwa Kaini na Abel. “Kaini alimuua ndugu yake na Mungu akamwambia atubu dhambi, akawa mkaidi kwa sababu alikuwa na roho ya shetani na matokeo yake alipata shida,” alisema Padri Magabe.  Aliwataka waombolezaji kushirikisha w...